MCHEZAJI LIGI KUU ENGLAND ATIWA MBARONI NA POLISI KWA KISA HIKI


Ikiwa ligi kuu ya England imeanza, headline sio nani kamfunga nani tu, bali hata maisha ya mastaa wa EPL nayo pia yana-make headline.
 Hivi sasa mchezaji wa West Ham Diafraa Sakho ana mashitaka polisi kwa kosa la kumshambulia mwanamke.
Kisa hiki kilitokea siku tatu kabla ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Arsenal ambapo walishinda kwa magoli 2 bila. 
Sakho alicheza karibia mechi yote dhidi ya Arsenal.
Diadra ambaye alinunuliwa kwa £3.5m mwaka jana alikamatwa kwenye nyumba yake huko Essex na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha East London. 
Makosa yake yameandikwa kuwa ni kusababishia majeraha na kumtolea lugha chafu mwanamke huyo.
Japokuwa taarifa hiyo ya polisi haikusema mwanamke huyo ni nani, ripoti za ndani zinasema atakua mpenzi wake  anayeitwa Maya.
Hata hivyo, Msenegal huyo ameachiwa huru kwa dhamana, huku akitakiwa kurudi kituo mwishoni mwa mwezi ujao.
poli

Related Posts