TAMWA: Serikari isimamie haki


Serikali imetakiwa kusimamia haki za binadamu ipasavyo na kuzifuatilia kwa ukaribu na kutoa adhabu kali ili kuondokana na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia ususani kwa watoto, wananwake na walemavu wa ngozi.
Hayo yalisemwa na Wence Mushi mwezeshaji kutoka katika chama cha waandishi wa habari wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoa mine yaliyofanyika mkoani iringa na kubainisha kuwa bila sheria za binaadamu kusimamiwa kikamilifu bado unyanyasaji utazidi kuendelea nchini.
“Kama sheria za haki za binadamu hazitasimamiwa vizuri na maafisa usitawi wa jamii bado ukatili wa aina yoyote utaendelea katika mazingira tunayoishi,hadhi ya wanawake na kuonekana kama ni chombo cha starehe itaendelea kwa sababu haki hazisimamiwi ipasavyo”alisema Mushi
Mushi aliwataka wanahabari kuendelea kuibua mambo ya kikatili yanayofanywa na baadhi ya watu hasa kwa watoto, wanawake na walemavu wa ngozi ili kuipa elimu jamii na kushinikiza serikali kuchukua hatua katika ukatili huu.
“kuna taasisi na mashirika yanayojihusisha na kutetea haki za watoto hivyo ni vyema waandishi kila wanapoona matukio kama hayo yanatokea wakayaibua ili kuyatokomezakwa kuchukuliwa hatua”aliongeza.

“Ni dhahiri kwamba kuwa vitendo vya unyanyasaji vimepungua kutokana na wanaofanya ukatili huo kuelewa, na watendewa pia kuzidi kuamka, juhudi zaidi zilitakiwa kujipenyeza zaidi dhidi ya imani za kimila ambazo bado zinashikiliwa katika sehemu mbalimbali za nchi.”alisema Mushi

kwa upande wake mwanahabari  Geofrey Nilahi kutoka gazeti la Tanzania daima songea alisema kuwa wanahabari ni chachu ya mabadiliko kama tukiibua mambo ya kikatili yanayofanywa na kushinikiza yafanyiwe mabadiliko hasa katika usimamizi wa sheria na kuchukuliwa hatua kwa waharifu.
“wanahabari ni chombo muhimu sana na ili kutokomeza ukatili wa ainayoyote ni lazima kalamu zetu zitumike kukemea mambo yasiyostahili kutedwa na kufuata haki za binadamu ili kuleta usawa katika jamii”alisema

Festo Sikagonamo mwakilishi wa ITV mbeya alisema kuwa endapo wanahabari wakiwezeshwa na  TAMWA kufuatilia habari juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na mauwaji ya watu wenye ulemavu hakika mabadiliko yatakuja kupitia kalamu zetu.zitaleta mabadiliko makubwa hapa nchini.

Kwa upande wa waandishi wa habari wa Nyanda za Juu Kusini walioshiriki warsha hiyo walisema kuwa wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu,hivyo kuwaomba TAMWA kuwasaidia chombo cha usafiri kila mkoa ili waweze kuwafikia wananchi waliopo hasa maeneo ya vijijini.

Hata hivyo aliwataka  wanahabari  kufanya kazi kwa kufuata weledi na maadili ya kazi yao.