Na MatukiodaimaBlog
JESHI la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Iringa watumia mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi zaidi ya 60 wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema ) akiwemo mgombea ubunge wao jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa matatani kwa kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Iringa na wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa mgombea Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.
Baada ya polisi kufatua mabamo mawili ya machozi kwa ajili ya kusambaratisha wafuasi hao baadhi yao walikimbia huku mgombea ubunge huyo Mchungaji Msigwa akienda kujisalimisha mwenyewe polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo kabla ya kukamatwa na polisi.
Imeelezwa kuwa wafuasi hao ambao wengi wao ni vijana walikuwa wamekutana katika eneo la kambi ya kampeni ya Chadema iliyopo eneo la Hoteli ya Sambala jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa ajili ya kikao cha ndani toka majira ya mchana na jioni ndipo walipofanya vurugu hizo wakati wananchi wakitoka katika mkutano wa kampeni za mgombea huyo wa Urais wa CCM.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Rmadhan Mungi aliwaeleza jana waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12;30 jioni baada ya wafuasi hao kufunga barabara kuu ya Iringa –Dodoma na kufanya vurugu hizo kwa kuwarushia mawe wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa kampeni za Dr Magufuli uwanja wa Samora.
Alisema kuwa wakati jeshi la polisi likiwa katika mkutano wa mgombea huyo wa Urais wa CCM walipokea taarifa kuwa kuna vijana wa boda boda zaidi ya 150 walikuwa wakijikusanya kuelekea katika eneo hilo la Sambala Lodge na baada ya kufuatilia ndipo walibaini kuwa wanakwenda katika kikao chao cha ndani na kwa kawaida jeshi la polisi halikatazi watu kufanya vikao vyao vya ndani .
“Jeshi la polisi halizuii wanachama wa chama chochote cha siasa kufanya vikao vya ndani kwani ni haki yao ya kisheria na kikatiba …..lakini baada ya kikao chao kumalizika vijana hao walitoka nje ya ukumbi huo uliopo kando kando ya barabara na kuanza kufunga barabara na kucheza muziki katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa barabara kushindwa kupita ……baada ya vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU kwenda kuwatoa watu hao barabara ila walipuuza na kuishia kumpiga mawe na baadae kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya Sambala eneo ambalo wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema “ alisema kamanda Mungi.
Alisema wakati wa vurugu hizo baadhi ya vijana waliumia kwa kuruka ukuta na wengine kwa kuanguka wakati wa kujaribu kukwepa kukamatwa na kuwa wale wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa na kuwa miongoni mwao yumo mgombea ubunge jimbo hilo Mchungaji Msigwa .
Mbali ya mchangaji Msigwa wengine waliokamatwa kwa tuhuma za vurugu hizo ni pamoja na mgombea udiwani kata ya Gangilonga ambae pia ni mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo
Kamanda Mungi alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upelelezi kumamilika alisema kuwa mchungaji Msigwa hakuwepo katika eneo la tukio wakati vurugu hizo zikitokea ila ameingizwa katika orodha ya watuhumiwa kwa wakosaji wakuu wapo makundi manne likiwemo moja la yule anaendenda kosa kwa mikono yake ,kundi la pili muwezeshaji au mshauri na kundi la nne kutoa hamasa kwa wakosaji hivyo alisema mgombea huyo anashikiliwa kwa kutuma za kutoa hamasa kwa watuhumiwa hao kufanya vurugu.
Wakati huo huo jeshi hilo la polisi limepiga marufuku vyama vyote vya siasa kuwahamasisha wafuasi ama wanachama wake kufanya vurugu za wakati huu wa kampeni na kuwa kamwe jeshi hilo halitamvumilia kiongozi ama mtu yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani.
“Amani ni kitu cha kwanza na yeyote anayetishia kuvuruga amani ya Iringa anatishia kazi za polisi Iringa kamwe hatavumiliwa zaidi ya kuchukuliwa hatua kali na kuwataka vijana kuepuka kutumiwa na wanasiasa kufanya vurugu “
Kuhusu mwenendo wa kampeni toka zianze alisema kuwa hadi sasa tupo nusu ya kampeni hizo toka zianze na kuwa toka tarehe 22 hadi 30 mwezi wa nane hakukuwa na kosa lolote lililoripotiwa kutokea kuhusiana na kampeni ila tarehe 1 hadi 5 mwezi wa tisa kulikuwa na makosa 9 yaliyoripotiwa kituoni na tarehe 5- 19 kulikuwa na makosa 17 yaliyoripotiwa na makosa 15 yalitokea jimbo la Iringa mjini na makosa mawili wilaya ya Mufindi huku katika wilaya ya Kilolo hakuna kosa hata moja
Hivyo amewataka wagombea na wafuasi wao kufuata maelekezo yaliyomo katika kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichotolewa na tume ya Taifa ya uchaguzi .
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa fecaboook alithibitisha kukukamatwa kwa vijana hao na kiongozi wa kambi hiyo Bw Igogo wakiwa katika ngome hiyo ya kampeni.
By MichuziBlog