Mengele: tutawaambia wananci wasipige kura maoni Katiba

ASKOFU  wa kanisa la kiinjili la kiruteli hapa Tanzania (KKKT) Diosisi ya kusini, Isaya Mengele, amesema kuwa kama katiba haita wafikia wananchi kote nchini watatangaza kuto pigia kura katiba pendekezwa kwa kuwa mpaka sasa haijaanza kusambazwa kwa wananchi.

Alisema kuwa yeye amezunguka sehemu nyingi hajaona mahali ambapo wananchi wanasema wanaifahamu katiba hiyo kwa kuwa wanatakiwa kuisoma na kuielewa ili kupiga kura kwa kile walicho kisoma na kukielewa.

“Sisi kama kanisa hatutakubali kuwaruhusu wananchi kupigia kura Katiba pendekezwa kama haita fikishwa kwa wananchi, kwani wanatakiwa kuisoma katiba na kuielewa kabla ya kuipigia kura, endapo itafika tarehe 30 mwenzi wa nne tutawaambia wananchi wasiipigie kura na wasubiri waisome kwanza ” alisema Askofu, Mengele.

Alisema kuwa kanisa linajiuliza itakapo fika Aprili 30 wananchi watapigia kura ya ndio au hapana juu ya nini wakati hawajui kilichopo ndani ya katiba hiyo kiukweli hawata kubalian ana kitu hicho.

Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuielewa ili wanapo piga kura wajue nini nini wanacho kipigia kura wakati wa kupiga kura na kuwa watatangaza kwa umma wote ulimwenguni wajue na watawakataza kupiga kula.

Alisema kuwa wataungana na watanzania wote kuhakikisha serikali kuwa kunakuwapo kwa amani wakati wate wa mchakato wa katiba na uchaguzi mkuu.

“Sasa mwezi Januari karibu unaisha lakini uandikishaji wa kupiga kura haujaanza na mda uliopo ni mfipi kweli na rais alikutana na maaskofu tuka mshauri kuwa apitishe mchakato huo mpaka uchaguzi upite lakini alishawishiwa na bunge la maalum katiba (BMK) na kutangaza kufanyika upigiaji wa kula kabla ya uchaguzi mkuu wakati wa kupokea katiba pendekewa” aliongeza.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba, afisa tarafa ya Njombe, Lilian Kembele, alisema kuwa serikali inampango mkakati wa kuhakikisha inasambaza katiba pendekezwa kwa wanachi kabla ya kufika mda wa kuibigia kura.
Kembela alisema kuwa wanasiasa wawe makini katika kipindi hiki cha kuipigia kura katiba mpya na kuwa wasije wakaiingiza nchi katika machafuko kwa kuwashawishi wananchi kwa namna yoyote ile.

Alisema kuwa serikali haita kuwa na jinsi kama viongozi wa dini watawasimamisha wananchi kuipigia kura katiba hiyo na kuwa kwa kuwa ipo ile ya zamani serikali itaitumia ile ya zamani na kuendelea na mchakato baada ya kumaliza vikwazo.