Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika tamasha
la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam na kuahidi
kutoa sh. milioni 6 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Msama
alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari
Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
Mjumbe
wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASAT) Alex Msama ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions akizungumza katika tamasha la Uimbaji na
Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Msama alikuwa mgeni
rasmi katika tamasha hilo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika tamasha
la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Msama alikuwa
mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana
Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
Mchungaji Emmanuel Masanja 'Masanja Mkandamizaji' aliguswa na kutoa ahadi ya shilingi milioni 1 katika hafla hiyo.
"Mimi na familia yangu tutatoa milioni 1".
Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi, Mchungaji
Christosiler Kalata akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotions, Alex Msama sehemu ya mchango walioahidi katika tamasha la
Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Usharika huo
ulitoa ahadi ya sh. laki 7.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akipokea mchango wa
Usharikia wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi kutoka
kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Christosiler Kalata .
Familia mbalimbali ziliguswa na kutoa ahadi za kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.
Watu mbalimbali waliahidi kutoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Edson Mwasabwite alichangia kiasi cha sh. laki moja.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MJUMBE wa Baraza la Sanaa la
Taifa (Basata), Alex Msama ametoa kitita cha sh. mil 6 katika harambee
ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika
Segerea.
Msama ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika hafla hiyo, alitoa kiasi hicho katika harambee hiyo ya kufanikisha
ujenzi huo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam,
huku akitoa na ushuhuda wa maisha yake mpaka kufikia hatua aliyofikia sasa.
Akizungumzia ushuhuda huo,
Msama aliwataka waumini kuiga mfano wake kwa kujitolea bila ya kugeuka nyuma,
kwani ana imani Mungu yupo na anatenda muujiza kama alioutenda kwake.
"Unajua mimi katika
maisha yangu hakuna ninayemwamini zaidi ya Bwana Yesu, kwa kuwa bila ya yeye
mie nisingekuwa hapa nilipo, kwa taarifa yenu wapendwa mimi nilishakuwa dereva
taxi, nilishakuwa kondakta wa daladala, lakini Mungu ni mwema na anatenda
muujiza mpaka mimi kuwa hivi," alisema Msama.
Msama ambaye ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions, aliongeza kuwa hata hivi karibuni katika ajali
aliyoipata akienda Dodoma licha ya kupinduka gari mara nne lakini alitoka akiwa
hai.
Harambee hiyo iliyoenda
sambamba na mnada, ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili kama
Masanja Mkandamizaji, Edson Mwasabwite aliyeimba wimbo wa Ni kwa neema tu.
Mbali ya kiasi hicho
alichotoa, Msama pia alichangia katika mnada uliofanyika katika tamasha hilo na
kununua mtungi wa gesi kwa sh. laki 5.