MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe, Antony Mahwata, jana alipandishwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe kufuatia kesi inayo mkabili ya kutishia kumuua mbunge wa zamani wa jimbo la Njombe Magharibi na kutakiwa kuanza kijitetea.
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Njombe Augustine Lwinzile alisema kuwa mshitakiwa hiyo akiwana mwenzake baada ya kusikiliza upande wa mashitaka imebaini kuwa washitakiwa wanakesi ya kujibu kesi hiyo kwa upande wa serikali inasimamiwa na mawakili wa serikali Happiness Makungu na Epct Atupakisye Mwakasitu.
Alisema kwa kuwa mahakama imeona washitakiwa wana kesi ya kujibu na kusema kuwa washitakiwa wanaweza kuanza kujitetea.
Hakimu aliwauliza washitakiwa kiwa kama kuna haja ya kuwa na mashahidi katika utetezi wao mshitakiwa wakwanza aliiambia mahakama kuwa katika utetezi wake atakuw ana mashahidi watatu watakao simama upande wake.
Alivyo ambiwa aanze kujitetea alisema hayuko tayari kwa siku hiyo na kuiomba mahakama kuwapangia siku nyingine kwaajili ya kusikiliza kesi yao.
Kwa upande wake mshitakiwa wa pili Evaristo Mahurumi alisema kuwa yeye katika kesi hiyo atakuwa na mashahidi wawili na kuwa hayopo tayari kwa kujitetea siku hiyo huku akiiomba mahakama kupanga siku nyingine ya kusikiliza kesi hiyo.
Washitakiwa hao waliulizwa na mahakama hiyo kama watakuwa na vielelezo vya kujitetea katika utetezi wao waliiambia mahakama kuwa hawata kuw ana kielelezo hata kimoja .
Kesi hiyo inawakabili washitakiwa hao dhidi ya mbunge mstaafu Stanley Yono baada ya washitakiwa kushitakiwa kwa kosa la kumtishia kumuua.
Mahakama imeahilisha kesi hiyo mpaka Octoba 23 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena na washitakiwa wakipewa nafasi ya kujitetea dhiti ya mashitaka yanayo wakabili.
Mwisho.
Habari Online na Elimtaa
MAHAKAMANI NAKO
Kesi ya Antiny wamwenyekiti halkmashauri wangingombe yapigwa kalenda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)