Baadhi
ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya nchini
Marekani waliokuja nchini kwa lengo la kutizama fursa za uwekezaji.
Afisa
wa Ubalozi wa Tanzania nchini Washington DC,Suleiman Saleh (katikati)
akibadilishana mawazo na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme
ya TANASI ,William Crawford.Ziara hiyo inayo ratibiwa na Ubalozi wa
Tanzania,Washington DC ni ya siku ambapo wageni hao wataembelea sehemu
mbalimbali kujionea fursa za uwekezaji.
Afisa
Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC ,Suleiman Saleh akizungumza juu ya
ujio wa wageni hao 11 kutoka Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya
kutizama fursa ya uwekezaji.Hii ni mara ya tatu sasa Viongozi wa
Makampuni mbalimbali ya Marekani wanafika nchini ikiwa ni utekelezaji
wa mpango wa Rais Kikwete kutekeleza Dipromasia ya Uchumi.
Rais
wa Kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc ,Ahmed Issa,ambaye pia ni
Balozi wa heshima akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya
Mount Meru, jijini Arusha kuhusu ujio wa Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi
wa makampuni mbalimbali ya Marekani walioko Tanzania .Issa tayari
ambaye ni ziara yake ya tatu sasa kuja Tanzania tayari ameanza uwekezaji
katika sekta ya Utalii ikiwemo kufungua ofisi ya Utalii Carfonia
Marekani iliyozindiliwa hivi karibuni na Rais JAkaya Kikiwete.
Mtaalamu
wa Ujenzi wa nyumba za makazi ,Nishati Erick Nyaren akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu ujio wao Tanzania .Nyaren yuko nchini
kuangalia fursa katika uwekezaji katika sekta ya Ujenzi. na Miundo
mbinu.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na
mjukuu wake Colin Machamsoc akizungumza na wanahabari kuhusu ziara yao
ya siku sita nchini Tanzania ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii vya
,Manyara,Serengeti na Ngorongoro.Crowford yuko nchini kutizama fursa ya
uwekezaji inayopatikana katika sekta ya Kilimo.
Mhandisi
wa vifaa vya matibabu,Bob Reynolds akizungumza na waandishi wa habari
namna anavyofikiria kuwekeza katika sekta ya Afya hasa kwa kutizama
upatikanaji wa vifaa tiba kama X Ray,Ultrasound na CT Scan.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na
mjukuu wake Colin Machamsoc wakiwa katika pozi la Picha katika hotel ya
Mount Meru.
Marais,Wenyeviti
na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya Marekani wakiwa katika picha
ya pamoja katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.Na Dixon Busagaga wa
Globu ya jamii
kanda ya kaskazini.