Aadhibiwa kwa kusujudu uwanjani


Mchezaji wa Kansas City Chiefs Husain Abdullah aliadhibiwa vikali na refarii baa da ya kupiga sijida baada ya kufunga bao katika mchezo wa soka ya Marekani Kansas walipoinyuka New England Patriots 41-14.
Refarii alimwadhibu papo hapo Abdullah alipoinuka baada ya kusheherekea kwa kupiga sijida.
Aliyekuwa refarii wa zamani wa NFL Mike Pereira alisema kuwa sio hatia mtu kupiga sijida.
Tukio hilo linawadia wakati ambapo ligi hiyo inapigwa msasa kufuatia utovu wa nidhamu mbali na tuhuma chungu nzima kuhusiana na wachezaji wa ligi hiyo.
Tayari wandani wa NFL wanadai kuwa kuna upendeleo kwani mchezaji mwengine nyota Tim Tebow hakuadhibiwa baada ya kuonesha ishara yake al maarufu “Tebowing” msimu wote wa mwaka wa 2011.
Abdullah amejitokeza kutetea dini yake ya Uislamu sawa na vile Tebow huonesha wazi kuwa ni Mkristo.
Aidha Abdula alihiji mwaka uliopita alipoambatana na kakake Hamza,kuenda kwa hajji huko Mecca.
Kwa mujibu wa washika dau wanaishauri NFL itangaze wazi msimamo wake kuhusiana na ishara za kidini ilikutoa utata unaoibuka .