TIMU ya Bodaboda kata ya Njombe mjini imefanikiwa kuifunga mabao 4-1 timu ya bodaboda kata ya Mjimwema mkoani jombe katika bonanza la michezo lililofanyika Jumapili hii mwishoni mwa wiki iliyo pita.
Bonanza hilo lilillojumuisha michezo miwili ya mipira wa miguu kwa timu za wanawake kutoka mjini Makambako na timu za mpira wa miguu wa wanaume waendesha bodaboda kutoka halmashauri ya Njombe.
Michezo hiyo iliyotoa iliyo fanyika mkoani Njombe waendesha bodaboda, wa kata ya Njombe mjini wamefanikiwa kujinyakulia kikombe kilicho andaliwa na Mtabibu wa tiba mbadala, Dr. Haja Hussen Mpapai, ambayo yamegharimu zaidi ya shilingi milioni 2.
Akizungumza katika mashindano hayo baada ya kukabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza kwa madeleva bodaboda kata ya Njombe mjini kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Wilibroad Mtafungwa, SSP Nicodemus Katembo, alisema kuwa mashindano hayo yameisaidia jamii kuwa pamoja na kuwa kupitia mabonanza matatizo yanaweza kutatuliwa.
Alisema kuwa kupitia michezo hiyo jamii huachan ana vishawishi vya kutenda maovu kutokana na kushiriki michezo na kuhakikishiwa afya bora baada ya michezo.
Kwa upande wake Mwandaaji wa bonanza hilo Dr. Mpapai alisema kuwa mashindano yayo maanda lizi yake yamegharimu zaidi ya shilingi Milioni 2 huku akisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa jamii inaboresha afya zao na kimarisha undugu.
Alisema mashindano kama hayo yanasaidia kuinua vipaji wa wachezaji na kuwa atahakikisha kuwa anaweka mabonanza mengi ili kuhakikisha kuwa jamii inaona matunda ya kuwa na wanamichezo na kuwa viongozi mbalimbali amewahimiza kuanzisha mashindano ya michezo ili kuwaondoa