NAPE AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA MAGOMENI WILAYA YA BAGAMOYO


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Bagamoyo alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Magomeni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa shina la wakereketwa la stendi ya Kangowe mara baada ya kulifungua shina hilo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma ya asili ya watu wa Bagamoyo kabla ya kuanza kuhutubia wakazi wa kata ya Magomeni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo kwenye viwanja vya shule ya msingi Majengo na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu kwa kumchagua mgombea kutoka CCM kwani ndio chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa
 Wapenzi na Wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi wakijumuika kucheza ngoma ya asili ya Bagamoyo.
 Mgombea wa Kiti cha Udiwani Kupitia CCM Mwanaharusi Hamis Jarufu akipiga magoti kwa wapiga kura wake kama ishara ya kuomba kura.
 Mgombea wa Kiticha Udiwani kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo kwa tiketi ya CCM Mwanaharusi Hamisi Jarufu akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wakati wa uzinduzi wa kmapeni za udiwani wa kata hiyo.
Na Maisha Kiasi Blog