Muigizaji nguli wa Sinema nchini India Suchitra Sen amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na maradhi ya kifua.
Mwana filamu huyo alilazwa hospitali nchini humo
kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na matatizo kifua lakini bado hali
yake ilizidi kuzorota zaidi jana usiku na kisha kumsababishia kifo.Alikuwa miongozi mwa waigizaji nguli kati ya waigizaji wa Bengali, aliungana na waigizaji wengine kama Uttam Kumar na wakaweza kutengeneza mfululizo wa filamu iliyochukua miongo miwili.
Baadhi ya waigizaji waliowahi fanya kazi na Sen wanamuelezea kuwa alikuwa ni mtu wa tofauti na mwenye kipaji kikubwa katika fani ya uigizaji.
Sen alianza uigizaji 1953 na filamu yake ya kwanza ilikuwa Seventy-four-and-a-half ambayo yeye aliigiza kama muuguzi na kuonekana kumudu sana nafasi hiyo.
Familia ya Sen ni waigizaji akiwemo mtoto wake wa kike Moon Moon Sen na wajukuu zake Riya na Raima Sen.
Na BBCSwahili