MTOTO Enjo Maklin (4½) amefariko dunia wakati akipatiwa
matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya baada ya kugongwa na Lori
barabara ya Tukuyu – Mbeya.
Akitoa taarifa kwa
waandishi habari Mkoani Mbeya Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa
mtoto huyo aligongwa na Lori, Jana majira ya saa 9:30 mchana maeneo ya Itezi
jijini Mbeya.
Alisema mtoto huyo
amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
mdamfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Masangi alisema
kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyo sababishwa na Lori aina ya scania lililokuwa likiendeshwa
na Abbulahamani Ally (35) mkazi wa jijini Dar es Salaam ni mwendo kasi.
Alisema mwili wa
mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali hiyo ya Rufaa.