LORI aina ya Volvo limepinduka na kusababisha kifo cha
dereva papo hapo katika maeneo ya Ilongo wilayani Mbarali Mkoani Mbeya baada ya
kuacha njia barabara ya Mbeya – Njombe jana.
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi
akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana
majira ya saa 6:00 alasili katika maeneo ya Ilongo wilayani Mbearali mkoani
Mbeya.
Alimtaja marehemu huyo kuwa ni Abdul Karim (40)
Mkazi wa Jijini Tanga, na alikuwa akiendesha gari yenye namba za usajili namba T.554
BDQ na Tela namba T.106 BFD.
Alisema kuwa lori aina ya Volvo liliacha njia
na kupinduka kisha kusababisha kifo cha dereva wa gari hiyo papo hapo.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni Mwendo kasi
wa hali hiyo, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitari ya Rufaa Mbeya