JOHN
Malecela atokauli juu ya gumzo la mbio za kuelekea urais mwaka 2015 linalo endelaa ndani ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) na amempongeza Paul Makonda kwa kauli anazozitoa.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Malecela alisema kuwa ameamua kusema
na kutoa kauli kuhusiana na watu wanaoendelea kuzungumzia suala la mbio za
kuelekea urais mwaka 2015.
“Ndugu
waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha
ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa
watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu
cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni
baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana
Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na
baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana
kijana huyu,” alisema Malecela.
Alisema kuwan
anadiriki kusema ampongeza kijana huyo hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri
kwa maslahi ya CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.
Alisema kuwa
itakuwa si busara kama hatawapongeza vijana wake katibu mkuu wa chama ndugu Abdulrahman
Kinana na Nape Nnauye kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea
kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa
bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee
-na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watu
wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na
serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.
Aidha aliwaomba
watanzania wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache
wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani,
upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba wa taifa mwalimu
julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la Afrika.
Alisema kuwa
msemaji wa UVCCM, Paul Makonda anamuunga mkono kwa kitendo chake cha ujasiri
cha kumkemea ndugu Edward Lowassa bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama kwa
lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati
inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka
misingi na katiba ya chama.
Alisema “Hapa
najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi
iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?,.”
Ukweli ni
kwamba wanachama na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au
karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.
Alisema kuwa
bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa
lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu
misingi bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi ndani ya chama hicho.
Aliongeza kuwa
kinachomsikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya
juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu Abdulrahmani
Kinana na katibu mwenezi Nape Nnauye za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.
Malecela aliomba
juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama, Ukweli ni kwamba vijana
hao wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama kwa wananchi kila
pembe ya taifa kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora.
Swali: Je!
Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?
Aliongeza kwa
kusema “Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri secretariet
ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema
haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza
sana”.
Vijana na
wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo
wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya wengine kupoteza
mwelekeo.
Walikijenga chama
hicho kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake
kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa
maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi
ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka
kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka wanashangaa na kujiuliza
hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi
ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.
alitoamfano
hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye
vyombo vya habari, vitendo hivi havikuwa na tija kwa chama na wala havileti
umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama hicho kwa muda mrefu.
“Ninaomba
sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli
kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta
kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima,” alisema Malecela.