CONTACT WITH ELIMTAA BLOG BY: CALL :+255 788 056115 EMAIL: furahanews1@gmail.com Facebook: www.facebook.com/elimtaa Twitter: www.twitter.com/@elimtaa "ANY TIME CALL US FOR ADVERTISEMENT, OR ANY NEWS YOU WANT APPEAR TO Elimtaa Blog" Elimtaa 'more news update your mind'
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF),
Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri,
baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao
ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Alisema chama chake, kina wasiwasi na
elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo
alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala
ya biashara.
Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu
wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na
kuhitimu kidato cha sita.
Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi
chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo
aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara
hiyo nyeti.
“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona
wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule
alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua
na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo
linatia mashaka,” alisema Lipumba.
Alisema nafasi aliyopewa inahitaji
kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu
uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za
ndani na nje ya nchi.
“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya
Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza
kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina
mashaka,” aliongeza.
Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye
vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi,
kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na
ufahamu wake.
WAZIRI AJIBU
Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu
madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani
alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini
Zanzibar.
Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya
diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia
alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.
Alisema mbali na masomo hayo, pia
amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
(OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.
“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu
(PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar
es Salaam,” alisema Mkuya.
Na Udakuspesial
Subscribe to:
Post Comments (Atom)