WATU
watatu akiwemo Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Newala, ASP-Nurdini
Kassim Seif (38) wamefariki dunia kufuatia ghasia zilizojitokeza jana
((12.1.2014) katika Kijiji cha Kiduni Kata ya Mtonya Tarafa na Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara.
Hayo yamebainishwa leo
na Issa Mnilota (ACP) ofisini kwake kwa niaba ya Kamanda wa polisi Mkoa
wa Mtwara Zelothe Stephen wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa
kuhusiana na tukio hilo kuwa, tukio limetokea mnamo majira ya saa 16:45.
Aidha, amewataja
marehemu hao kuwa mwananchi mmoja aliyetambulika kwa jina la Hamza
Msangaluwa ambaye amefariki baada ya kupigwa risasi ya kichwa , Mkuu wa
upelelezi ASP-Nurdini Kassim Seif (38) na F.8106 DC Rogert ambapo wote
walikufa papo hapo baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali ikiwemo
kifuani, tumboni, mapajani na miguuni kufuatia vurugu hizo.
Aidha waliyoshmbuliwa
ni F.5339 (33) na PC Issaya (34) ambapo PC Issaya amejeruhiwa vibaya
sehemu ya paja ambapo kwa sasa yuko katika Hospitali ya Wilaya ya Newala
kwa matibabu zaidi.
Vurugu hizo zimetokea
nje kidogo ya Mjini wa Newala umbali wa km 5 barabara ya Newala – Mtwara
ambapo jambazi mmoja akiwa na silaha inayosadikiwa kuwa
SMG alikwenda kituo cha mafuta cha Camel akiwa amebeba galoni na kununua
mafuta ya Tshs. 2500/= na kuweka kwenye galoni alokuwa amebeba.
Mara
baada ya kupatiwa mafuta hayo aliingia ndani ya jingo la kituo hicho na
kuwataka wahudumu wampatie mauzo ya siku mbili yaliyofanywa kituoni
hapo ambapo wahudumu walimjibu kuwa hawana fedha, fedha zote
zimechukuliwa ndipo alipotoa silaha aliyokuwa ameficha ndani ya koti
alilokuwa amevaa na kuwalazimisha watoe fedha.
“Kufuatia hatua hiyo
jambazi huyo alianza kupekuwa na kuona fedha zilizokuwa uvunguni mwa
meza ya kituo hicho na hatimaye alifanikiwa na kuweka fedha hizo ndani
ya mfuko wa koti alilokuwa amevaa na kikumbilia vichakani”.Alisema
Mnilota.
Hata
hivyo wahudumu hao walianza kupiga kelele na kuomba msaada kutoka kwa
wananchi ndipo wananchi walianza kujitokeza na kuanza kumkimbiza na
wakiendelea kumfatilia kwa nyuma, jambani huyo alianza kuwafyatulia
risasai lakini wananchi waliendelea kumkimbiza kiasi cha umbali wa km 8
na kuingia kwenye kichaka.
Alisema
kuwa, polisi nao kwa muda huo walikuwa tayari wamepata raarifa na
kuelekea na eneo la tukio ambapo jambazi huyo akiwa amejificha kwenye
kichaka alifanikiwa ndipo akafanikiwa kumpiga risasi mwananchi huyo
mmoja ambaye ni marehemu baada ya kubaini alipokuwa amejificha jambazi
huyo hata hivyo jirani akiwepo Mkuu huyo wa upelelezi.
Aidha, jambazi huyo
amefanikiwa kutoweka gizani na kuacha helment, koti, raba moja na mzula
aliokuwa amevaa na mwili wa marehemu Hamza Msangalukwa tayari
umechukuliwa na ndugu zake kwa mazishi na miili mingine bado
imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo kwa taratibu zingine.
Alisema kuwa, jeshi la
polisi linatoa shukrani kwa wananchi wa Kijiji na Vijiji vya jirani na
watendaji wote wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano walioutoa na
wanaoendelea kuutoa kwa jeshi la polisi.
Aidha,
jambazi huyo amefanikiwa kuondoka na kiasi cha fedha Tshs. 3,299,180/=
ya mauzo toka katika kituo cha mafuta cha Camel na masako mkali wa
kumsaka jambazi huyo unafanyika na watatoa taarifa zingine zitakazo
patikana.
Pia
jeshi la polisi Mkoani hapa linatoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano utakaowezesha kuwabaini na kuwakamata wale wote waliohusika
na tukio hilo.
Na Kamanda wa matukio