KILIMANJARO:
Katika taarifa ya habari ya Radio Sauti ya Injili, Moshi jioni hii, imeripotiwa
kuwa watu watatu wamepoteza uhai huku wengine 30 wakiachwa na majeraha mbalimbali
wakati basi la kampuni ya Hood lenye namba T.497AHD walilokuwa wamepakia
kutokea Iringa kuelekea Arusha, lilipopata ajali majira ya saa 11 jioni kwa
kuacha njia na kuanguka katika eneo la Nkwini, huko Makanya-Hedaru katika
barabara ya Same-Mombo wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Majeruhi
wawili hali zao zimeelezwa kuwa mbaya hivyo kuwahishwa katika hospital ya rufaa
ya KCMC. Majeruhi wengine wawili walitibiwa katika kituo cha afya cha Hedaru
wakati miili ya marehemu waliotajwa na Robert Boaz (Kamanda wa
Polisi
mkoani Kilimanjaro), kuwa ni Stephano Kasimba, Fadhili Kasimba na Aziza Mdee,
imehifadhiwa katika hospitali ya Same ambako majeruhi wengine 25 wanaendelea na
matibabu.
Walionurusika
kifo wamesema basi hilo halikuwa katika mwendo ila dereva wake aliyetajwa kwa
jina la Baraka Juma, alionekana kuwa mchovu na huenda ajali hiyo imetokana na
usingizi uliomkumba dereva huyo ambaye ametoroka baada ya ajali hiyo kutokea.
LINDI:
Taarifa ya TBC Taifa iliyosomwa saa mbili usiku huu inasema kuwa, watu 9 wakiwemo
watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya
basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda
mkoani Mtwara kupinduka chana wa leo katika kijiji cha Mambulu huko katika
manispaa ya Lindi, wakati likipishana na lori kabla ya kupoteza mwelekezo na
kupinduka wakati mvua kali ikinyesha.
SINGIDA:
Imeripotiwa katika taarifa ya TBC saa saba mchana na mbili usiku uu kuwa jumla
ya abiria 13 wakiwemo watatu wa familia moja, wamefariki dunia mkoani Singida
leo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na
lori aina ya Scania T.687 AXB.
Ajali
hiyo ya mbaya iliyoacha miili ikiwa haitamaniki, imetokea leo mwendo wa saa
moja asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma kwenye eneo la kijiji cha
Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya
Noah lilikuwa likitokea Itigi kuelekea Singida Mjini huku lori lililokuwa
likitokea Mwanza kupitia Singida kuelekea Dar es Salaam, wakati likipishana na
Noah hiyo, lilihama upande wake na kuifuata Noah upande wa kushoto na kuigonga
na kuiburuza: “...baadhi ya watu wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisinzia
na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata Noah. Uchuguzi
utakapokamilika tutatoa taarifa hiyo,” amesema.
Hadi
sasa miili ya marehemu iliyokwishakutambuliwa na ndugu zao ni pamoja na Omari
Shaaban (44) na mkewe Salma Omari na
mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi Mjini. Haji Mohammed (29)
(Msisi), Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda), Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),
Samir Shaban (20) (Puma), Mwaleki Nkuwi
(35) (Ikungi), Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).
Miili
ambayo haijatambuliwa imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya mkoa, mjini Singida.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida, Dk. Banuba Deogratius amekiri
kupokea miili ya watu 13, wawili kati yao wakiwa ni watoto.
Katika
ajali hiyo, abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo.
Bofya hapa kutazama video ya ajali Singida (((((()))))))
Matukio haya yamekusanywa na www.wavuti.com