Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika
WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya fusu na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku huu wakati boda boda hiyo ikiwa katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia lilikuwa katika mwendo na kusababisha vifo hivyo .
Mashuhuda wamesema kuwa kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda hiyo ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado kutambuliwa .
Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi