WANANCHI wa halmashauri ya Mbeya wanatarajia kutufaika na uendelezwaji wa bonde la Mto Songwe unaonendelezwa kwa kujenga mabwa na serikali mbili za Tanzania na Malawi.
Mto huo unatarajia kuongeza kipato kwa wakazi wa halmashauri za Mbozi, Mbeya, Ileje na Kyela kwa Tanzania na baadhi ya halamshauri za nchini Malawi kwa kufanya biashara na kunufaika na umeme.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa mradi wa uendelezaji wa bonde la mto Songwe mwakilishi wa Tanzania, Eng. Gabriel Kalinga wakati akizungumza na madiwani wa Kata za Halmashauri ya Mbeya katika kikao cha baraza la madiwani.
Alisema wananchi wa halmashauri hiyo watanufaika kwa kujiingizia kipato na wengine kupata ajila katika sekta mbalimbali ikiwemo za uvuvi na utalii.
Alisema katika uendelezaji wa bonde hilo kutajengwa mabwa ambayo lengo lake itakuwa ni kupunguza athali zinazotokana na mafuriko na kuhamahama kwa mtohuo ambao umekuwa kero kwa wananchi wa maeneo ya jirani yam to huo kwa pande zote Mbili Tanzania na Malawi.
Kalinga alisema kuwa wananchi watajihusisha na uvuvi katika mabwa hayo ambayo kufugwa samaki na kuendesaha utalii ambao watalii watatembea kuzunguka katika mabwawa hayo yatakayo kuwa na mandhari nzuri.
Aliongeza kuwa mabwawa hayo yatakuwa matatu katika ambayo yatazalisha umeme utakao tumika katika nchi zote mbili na kupunguza tatizo la umeme vijijini.
Alisema kwa wananchi walio mabondeni watanufaika na kilimo cha umbagiliaji na kulima mazao mbalimbali na kukuza kipato chao kwa asilimia kubwa ukilinganisha na kipato chao kwa sasa.
Uendelezaji wa Mto Songwe umekuja baada ya mto huo kuwa na mazara kwa wananchi wanao uzunguka na kusababisha hasara zitokanazo na mafuliko.