WANAOTUMIA vyoo katika hospitali wametakiwa kuzitumia kwa umakini na usafi ili kulinda afya za watu wengine maeneo yanayo zunguka Hospitali na wao wenyewe.
Akijibu swali la madiwani wa kata za halmashauri ya Mbarali waliohoji uchafu uliotawala katika vyoo vya wagonjwa na vya wafanyakazi kuwa safi, Mkanga mkuu wa Halmashauri ya Mbarali, Dkt. Bonface Kasululu alisema kuwa wanachi wawe wasafi katika matumizi ya vyoo vya hospitalini.
Alisema kuwa baadhi ya wananchi wa halmashauli ya wilaya hiyo wanaopata huduma katika hospitali ya Rujewa wamekuwa wakitumia vibaya vyoo ya hospitalini hapo.
Kasululu alisema kuwa wananchi wanaoenda kupata huduma wamekuwa wakitumia karatasi ngumu pamoja na mawe katika vyoo badala ya kutumia maji baada ya kumaliza haja.
“Wananchi wamekuwa wakitumia karatasi na mawe baada ya kumaliza haja na kusababisha vyoo vya kutumia wagonjwa kuwa vichafu na kuziba mara kwa mara na wananchi wamekuwa wakitumia vibaya vyoo hivyo,” alisema Dkt. Masululu.
Aliongeza kuwa wananchi wengine wamekuwa wakitumia vibaya kwa kutojua matumizi na wengine wanatumia kwa makusudi kwani hawavipendi na wanahitaji vyoo vya shimo.
Huo ulikuwa ni ufafanuzi wa swali lililoulizwa kuhusu matumizi ya Jiki ambazo zilinunuliwa kwaajili ya usafi katika hospitali ya wilaya ya Mbarali, Rujewa Diwani wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Igurusi, Lucy Ng'ondo alihoji matumizi ya dawa hizo za usafi hospitalini hapo.
Alisema kuwa halmashauli ilitoa pesa za kununulia dawa za usafi hospitalini hapo na bado uchafu upo huspitalini hapo na kusema kuwa vyoo vya wafanyakazi vipo safi na vya kutumia wagonjwa vichafu.
Hivyo alisema kuwa hospitali ijitahidi kufanya usafi chooni hapo ili kuzuia watu wanao enda kupata huduma hapo wasije wakapata magonjwa badala ya kupata huduma ya afya hospitalini.