PALETO KUUNDIWA VITUO VYA UNUNUZI

MADIWANI wa halmashauri ya Mbeya wameamua wameitaka halmashauri hiyo kufungua vituo vya ununuzi wa Paleto katika maeneo ya mashambani ili kuzibiti makusanyo ya kodi.

Akihoji mapato yatokanayo na kodi za ununuzi wa paleto, diwani kata ya Maendeleo Daniel Nyamwale alisema kuwa takwimu za makusanyo ya kodi za mauzo ya Paleto zimekuwa zikitolewa zisizo sahihi. 

Hivyo ili kudhibiti hujuma katika makusanyo ya kodo hizo viundwe vituo vya kakusanyo ambapo wananchi wataenda kuuza hapo Paleto.

Kwa utaratibu unao tumika hivi sasa wa mnunuzi kwenda nyumba kwa nyumba kufanya manunuzi ya Paleto kunasababisha halmashauri kudanganywa.

"Mtindo unao tumika katika manunuzi ya Paleto kutoka kwa wakulima unasababisha takwimu za mapato yanayotokana na mauzo ya Paleto kuwa sio sahihi kutokana na wanunuzi kupita majumbani kwa wakulima," alisema Nyamwale.

Alisema hivyo ni rahisi halmashauri kudanganya na walipa ushuru kwani ni rahisi kukwepa kutoa ushuru na kufanya udanganyifu.

Hivyo halmashauri ifanye haraka kutambulisha mfumo wa kuwapo kwa vituo vya manunuzi ya Paleto ambapo wakulima watapeleka katika kituo kuuza Paleto na kutakuwa na mkusanyaji wa ushuru kituoni hapo.