WAFANYABIASHARA: UHABA WA SHILINGI NI CHANGAMOTO




WAFANYABIASHARA ya ubadirishaji wa fedha za kigeni katika mpaka wa Tanza nia na Zambia katika mji ndogo wa Tunduma mkoani Mbeya wamekuwa wakibabiliana na changamoto ya kuwapo kwa uhaba wa shilingi.


Wakizungumza na Elimtaa katika hafra fupi ya uzinduzi wa tawi la benki ya Commercial Bank of Africa (CBA), wamesema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto ya upungufu wa shilingi katika biashara ya kubadilisha fedha za kigeni.

Wafanyabiashara hao walisema kuwa wamekuwa wakizikosa fedha hizo au kuzikuta ambazo hazikidhi mahitaji yao kulingana na eneo hilo kuwa mpakani na fedha kubadilishwa kila mara.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Juma Kasm mkazi wa mjimdogo wa Tunduma na Mfanyabiashara ya kubadili pesa alisema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kukusa pesa za kuuza wanapo zihitaji.

Alisema ujio wa benki hiyo huenda ikawasaidia kupunguza changamoto hiyo kwani wingi wa benki huduma zitaboreshwa kwa kuwekeana changamoto benki kwa benki.

Alisema kuwa kuwapo kwa benki chache huduma huwa duni ongezeko la benki huongeza kuwapo kwa ubora wa huduma kwa watumiaji kwani kuna kuwapo kwa ushindani.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa CBA, Yohana Kaduma, alisema kuwa benki hiyo iutajitahidi kuhakikisha wananchi wa Tunduma wanapata wanacho kihitaji kwa wakati muafaka.

Alisema benki hiyo itajitahidi kuweka huduma zinazo endana na mazingira ya biashara ya Tunduma na kuhakikisha biashara ina songa mbele kwa wakazi wa Mji huo.

Nae mkuu wa wilaya ya Momba Abihudi Saidea alisema kuwa benki iweke huduma ambazo zinaendana na mahitaji ya wakazi wa wilaya yake.

Alisema kuwa wananchi wa maeneo ya Tunduma na wilaya yake kwa ujumla wanauhitaji mkubwa wa huduma bora ya kifedha kwa ajili ya kutunza fedhazao na huduma zingine zinazo husika na kifedha kwa wakazi wa wilaya hiyo.