SIFA YA CHAKULA CHA MOMBA KISINDIKWE HAPA


BENKI nchini zimetakiwa kuwekeza katika kuwasaidia wakulima mbalimbali ili waweze kusindika mazao yao katika maeneo yanakozalishwa ili kulinda ubora wa mazao hayo.

Akizungumza na wafanyabiashara katika hafula fupi baada ya uzinduzi wa tawi la benki ya Commercial bank of Africa, (CBA) katika mji wa Tunduma, Mkuu wa wilaya ya Momba, Abihudi Saidea alisema kuwa benki ziwawezeshe wakulima wa Mpunga wa wilayani humo kwa kuwapa mikopo.

Alisema kuwa wilaya hiyo imekuwa ikizalisha mpunga wenye sifa kubwa hapa nchini lakini wilaya hiyo haipati sifa kutokana na mpunga huo kusindikwa nje ya wilaya kutokana na kukosa uwezo wa kusindika wilayani humo.

Alisema wakulima wakiwezeshwa kwa kupewa mikopo katika kilimo chao na kuazishwa kwa mashine zitakazo wawezesha kusindika mpunga huo na kutoka ukiwa tayali ni mchele wilaya hiyo itapata sifa ya kile inacho kizalisha.

Mchele huo umekuwa ukishuka sabani ya ubora kutokana na kuto sindikwa ukiwa wilayani humo na huenda sifa kupewa wilaya nyingine unako sindikwa mchele huo.

Nae mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Yohana Kaduma, alisema kuwa benki ipo tayali kuwakopesha wafanyabiashara watakao kuwa tayali kuweza mashine ya kusindoka mchele huo.

Alisema kuwa kwa kuwa benki hiyo imefunguia tawi wilayani huo itajitahidi kuhakikisha inawasaidia wakulima wilayani humo kwa kuwapatia mikopo nafuu kwa ajili ya kukuza uchumi wa wananchi wilayani humo.

Wilaya ya Momba imekuwa ikisifika kwa kuzalisha zao la mpunga katika maeneo ya kamsamba ambapo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakichukua jumua mpunga kutoka huko na kuusafirisha na kuusindika nje ya wilaya hiyo.