SAIDEA: LETENI HUDUMA KULINGANA NA MAHITAJI YA WAKAZI



TAASISI za kibenki katika Mkoani Mbeya zimetakiwa kujikika katika kuweka bidhaa kulingana na mahitaji ya wakazi wa mazingira husika.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Momba, Abihudi Saidea wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya Commercial bank of Africa, (CBA), katika mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, alisema kuwa taasisi za kibenki ziangalie mahitaji ya watejawao kabla ya kufungua huduma.

Saidea alisema kuwa kumekuwa na taasisi nyingi za kibengi ambazo zimekuwa zikianzisha huduma ambazo haziendeani na wateja wake huzika na hiyo imekuwa ni changamoto.

Alisema kuwa katika wilaya hiyo kumekuwa  na shughuli mbalimbali za kibiashara na kilimo ambapo wananchi wanahitaji huduma za kibenki kuwa karibu.

Alisema kutokana na mji mdogo wa Tunduma ambapo limefunguliwa tawi la benki hiyo kumekuwa na biashara mbalimbali kutokana na mji huo kuwa mpakani hivyo benki zinatakiwa kuangalia uhitaji wabiashara zinazo patikana maeneo hayo.

Wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa wamekuwa wakipata shida katika biashara ya kubadilisha fedha kutokana na shilingi kuwa adimu katika mabenki ya eneo hilo lenye uhitaji mkubwa wa ubadilishaji wa fedha.

Mmoja wa wafanyabiashara wa maeneo ya mji mdogo wa Tunduma, Peter Sanga alisema kuwa wamekuwa wakipatashida kubadilisha fedha za kigeni kuwa za kitanzania kutokana na fedha za kitanzania kuwa chache zinapo hitajika.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Benk ya CBA, Yohana Kaduma alisema kuwa benki hiyo kwa kutambua uhitaji wa kubadilisha fedha katika mji huo wa Tunduma Beki inakitengo maalum cha kubadilisha fedha.

Alisema kuwa kitengo hicho cha kubadilisha fedha za kigeni watajitahidi kuleta fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya mji huo.