TSH 20,000 BANDIA ZAKAMATWA MBEYA KWA MKULIMA



  • NOTO MBILI ZAKAMATWA KWA MKULIMA
  • ALIKUWA ANATAKA KUFANYA MANUNUZI


JESHI la Polisi mkoiani Mbeya linamshikilia Mkulima Joseph Ngonyani (20) kwa tuhuma ya kupatikana na Noti Bandia zenye thamani ya 20,000.

Noti hizo zilikamatwa katika maeneo ya Mwanjelwa jijini Mbeya ambapo mtuihumiwa alikuwa akitaka kuzitumia katika manunuzi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na noti mbili za za shilingi 10,000 bandia alizo kuwa akitaka kuzitumia kwa manunuzi.
Alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa na askali walio kuwa dolia na msako ndipo walipo mkuta mtuhumiwa huyo akiwa na noti hizo.

Alisema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanywa ili mkondo wa sheria kuchukua nafasi yake.

Athumani ametoa wito kwa jamii ya watanzania na wafanya biashara kuwa makini na kufanya uchunguzi wa pesa wanapo nunua ama kuchukua chenji.