MZEE mmoja amekufa papo
hapo baada ya kugongwa na gari ambayo hajijafahamika katika maeneo ya Kijiji cha
Mbugani wilani Chunya mkoani Mbeya.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 1:30 jioni katika maeneo ya Mbugani tarafa ya Kiwanja
wilayani chunya ambapo gal;I isiyo fahamika ilimgonga mtembea kwa miguu, Omari
mwangosi (75).
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alisema kuwa gari
ambayo ilisababisha ajali hiyo ilitokomea kusiko julikana baada ya kutokea kwa
tukioa hilo.
Alisema kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ambayo ilisababisha kifo cha mzee huyo
papo hapo.

