UTATA umegubika katika uzito wa dawa za kulevya zilizokutwa tumboni mwa maiti ya mtu mmoja mkoani Mbeya, ambazo awali zilionyesha kuwa zilikuwa ni kilo moja na gramu 140, lakini baadaye zikaonekana kupungua na kubaki gramu 972. 85.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alithibitisha suala hilo na kusema dawa hizo zimepungua uzito wa
gramu 167.15.
Alisema
dawa hizo zilizokutwa tumboni mwa Kassim Mboya zilikuwa katika mfumo wa pipi
zilizokuwa 65, ambazo moja kati yake ilikuwa imepasuka na kuwa na uzito wa kilo
moja na gramu 140.
Kamanda
athumani alisema pipi hizo baada ya kufunguliwa zilikutwa zimepungua uzito na
kufikia gramu 972. 85 ikidaiwa kuwa uzito uliobaki ni wa karatasi za nylon.
Awali,
kijana huyo alikufa akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela, wakati akipatiwa
matibabu baada ya kuugua ghafla kutokana na pipi hizo kupasukia tumboni.
Kamanda
Athuman alisema dawa hizo awali hazikutambulika ni za aina gani, lakini baada
ya kufanyiwa uchunguzi na Mkemia Mkuu wa Serikali, imebainika kuwa ni aina ya Heroine.
Mtu huyo
alikuwa akisafiri kutoka Tanzania
na kuvuka mpaka kupitia Kasumulo, wilayani Kyela kuelekea nchini Malawi akiwa
katika basi lenye namba za usajili T 319 BLZ.
Alisema
akiwa mpakani hapo katika hatua ya ukaguzi, mtu huyo hakushuka katika gari,
ambako alikuwa amenyong’onyea kabla ya kumpeleka hospitalini na kufariki.

