KARIAKOO WAGOMA KUFUNGUA MADUKA


YAWA KAMA MBEYA 

WAFANYABIASHARA wa Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wamegoma kufungua maduka yao wakipinga bei kubwa ya mashine za  Kielektroniki  (EFD)  na kutozwa asilimia 18 inayokatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kila bidhaa inayouzwa.
Wafanyabiashara hao wamefikia hatua ya kugoma kwa maelezo kuwa serikali haikuwashirikisha wakati wa kuziazisha matumizi ya mashine hizo.
“Tumegoma kufungua maduka leo(jana) na hadi pale matatizo yetu yatakapotatuliwa na kikubwa tulichogomea ni asilimia 18 inayokatwa na TRA kwa kila bidhaa inayouzwa,” alisema Novaty Tarimo, muuzaji wa simu mtaa wa Narung’ombe na Msimbazi.
Tarimo aiambia Elimtaa kuwa , asilimia hiyo inayokatwa na mamlaka hiyo inauwa mitaji yao na wanawaomba wakae chini na wafanyabiashara hao ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.
“Kero za polisi na TRA kusimama barabarani kukamata mizigo, kuikagua na kuwaomba rushwa kwa madai kuwa risiti haiendani na bei ya mizigo,” alisema mmoja wa wafanyabiashara ya urembo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonge.
Bonge alisema, mashine hizo zimekuwa zikiuzwa bei kubwa ambayoinakaribia kuwa sawa na mitaji yao.
Akizungumza na waandishi wa habari  jana, Mshauri wa Jumuiya ya Wafanyabiasha  hao, Jonson Minja, alisema wafanyabiashara hao wamelalamikia kutoshirikishwa kwa mambo mbalimbali yanayowahusu na kuona kama wanadharaulika.

Minja alisema, wamemuomba Waziri wa  Viwanda na biashara Dk. Abdalah Kigoda   kuonana naye kwa lengo la kukaapamoja na kujadili changamoto zilizopo katika matumizi ya mashine hizo.

“ Wafanyabiashara hawana ugomvi na TRA  kwa kuwa mamla hiyo inatimiza matakwa ya serikali , na  serikali ndio inatakiwa kuwasikiliza na kujua changamoto za matumizi za mashine hizo,” alisema Minja.

Hata hivyo, aliwaomba wafanyabiashara hao kuwa watulivu wakati wakiendelea na majadiliano baina yao na serikali.

“ Tunaiomba serikali itusikilize namna ya uendeshaji wa mambo mbalimbali ya wafanyabiashara,”alisema.

Aidha alisema, wanaiomba serikali kuwaondoa wamachinga wanaofanyabiashara kwenye milango ya maduka na kuwafanya biashara kuwa ngumu