MZAZI WA ALIYEKUTWA NA VITU VINAVYO ZANIWA KUWA NI MADAWA AJITOKEZA





BABA mzazi wa mtu aliye kutwa na vitu vin avyo sadikika kuwa ni madawa ya Kulevya amejitokeza ili kuuchukua mwili wa marehemu huyo.

Mwili wa marehemu Kassim Said Mboya ulihifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya ukiwa unasubiliwa  ndugu wa marehemu na kuendelea kwa uchunguzi.

Akizungumza na NIPASHE Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani jana alisema kuwa baba M zazi wa marehemu amejitokeza ili kuutambua mwili wa Mwanae ili auchukue kwaajili ya mazishi.


Alisema kuwa mwili huo unge kuwa tarari umechukuliwa na  baba wa Marehemu kwa kuwa bado munaendelea na uchunguzi haujachukuliwa bado.

Alisema kuwa mwili huo unaendelea na kufanyiwa uchunguzi katika hospitari ya rufaa na jeshi hilo likiendelea kufaya upelelezi.

“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili na upelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili kuwakamata wahusika wengine” alisema Athumani.

Alisema kuwa baba huyo wa marehemu amejitokeza jana ili kuuchukua mwili wa marehemu mwanane na tayari kwa kuufanyia mazishi.
Alisema muchunguzi kikikamilika baba wa marehemu atauchukua mwili huo ambapo uchunguzi wa vitu vilivyo kutwa tumboni kwa marehemu utakamilika muda si mrefu.
Marehemu Kassim Said Mboya, alifariki mwishoni wa wiki iliyopota baada ya vitu vinavyo sadikika kuwa ni madawa ya kulevya kupasukia tumboni na kusababisha kifo chake.
Marehemu aliokuwa anatokea jijini Dar Es Salaam na kuelekea nchi ya Jirani Malawi na alifia katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela baada ya kuugua ghafla akiwa katika gali alilokuwa akisafilia kuelekea nchini humo.