- PF3 ILITOLEWA NA BABA WA MTOTO
SHAHIDI WALIKUWA BABA NA MAMA
- MSHITAKIWA AKIKANA MASHITAKA
ALIHUKUMIWA VIBOKO 10 MA KIFUNGO CHA MAISHA
- AMEKAA JELA MIAKA 13
AMEACHIWA KURU BAADA YA KUKATA RUFAA
MAHAKAMA Kuu ya
Tanzania Kanda ya Mbeya Imemuachia huru Izak Laiton (34) aliye \kuwa
amehukumiwa kifungo cha maisha Jela na kuchapwa viboko 10 kwa kosa la kubaka.
Mshitakiwa huyo ameachiwa huru juzi katika kumbi za mahakama
kuu ya Mbeya kufuatia sababu ambazo jaji Samweli Kalua amezitaja kuwa
zilimkandamiza mshitakiwa huyo.
Akizitaja sababu zilizo sababisha mshitakiwa huyo kuachiwa
huru Jaji Kalua alisema kuwa katika hukumu ya kesi ya mshitakiwa huyo shahidi
katika kesi yake ushahidi ambao ulitolewa ni wa Baba na Mama wa Mtoto aliye
bakwa bila ya kuwapo kwa ushahidi kutoka Hopitalini.
Alisema kuwa sababu nyingine kuwa ni Fomu ya polisi namba
tatu (PF3), ilitolewa na mzazi wa mtoto na pia mtoto aliye bakwa hakutoa ushahidi
mahakamani.
Jaji alisema kuwa katika kesi hiyo ushahidi ulitolewa na watu
watatu ambao ni Baba, Mama na Askali Polisi, ambapo mshitakiwa alipo hojiwa
alisema kuwa yeye haja baka na siku ya tukio hakuwepo Nyumbani.
Jaji Kalua alisema kuwa kufuatia kuwapo kwa kasolo hizo
mtuhumiwa ataachiwa huru na alimruhusu kurudi nyumbani kwake akiwa amekaa jela
kwa muda wa miaka 14 wakati akishughulikia rufaa yake.
Mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la
kubaka chini la kifungu cha sheria cha 130 na 131 kifungu cha 3 cha kanuni ya
adhabu ukurasa wa 16 iliyo fanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo Septemba1 mwaka
1999 wilayani Mbozi ambako alihukumiwa katika mahakama ya wilaya hiyo.
Mshitakiwa huyo baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo hakulizika
na kukata rufaa ambayo imemnasua katika kifungo hicho cha maisha jela na viboko
10.