§
MNAMO TAREHE 07.11.2013
MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA
MBEYA. KASSIM SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI
DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA
MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA –
AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI.
§
MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE
ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM MUECK MICHAEL, AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA
AINA YA JEANS,T-SHIRT MOJA NYEUSI,RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU,MKATE MMOJA ,MKOBA
MDOGO WA KIUNONI,VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI
MBILI SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA
MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§
AWALI BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI
KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA
TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA
NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA
GARI HUKU HALI YAKE YA KIAFYA
IKIZIDI KUDHOOFIKA.
§
WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI
AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU
ALIFARIKI DUNIA.
§
KUFUATIA DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI
ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI
AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA
TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI
YA PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.
§
TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI
YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA
UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO.
§
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO
TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI
WA MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA
UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
Picha na Mbeya yetu
|