Jeshi la polisi mkoa ni Mbeya limewafikisha mahakani watu 46
kwa makosa mbalimbali ya ya kufanya mikusanyiko kwa siku mbili za jana na juzi
wakati wa mgomo wa wafanyabiashara jijini Mbeya.
Akizungunza na waandishi wa habari kamada wa polisi mkoani
Mbeya amesema kuwa watu 46 wamefikishwa mahakamani kati ya watu 105 ambao
walikamatwa katika mgomo wa wafanyabiashara ambao waligoma kufungua maduka
wakizipinga mashine za kielekroniki za kutolea risiti.
Amesema kuwa amani ya wanambeya italetwa na wanambeya
wenyewe kwa kuhakikisha hawajichukulii sheria mkonono.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandolo amesema
kuwa wanambeya wanatakiwa kuwa na utulivu na kuhakikisha Mbeya wakati wote
kunakuwa na ambani kwani Vurugu zinahalibu mfumo mzima wa maisha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanya biashara amesema kuwa
viongozi wataenda kuwaamba wafanytabiashara wengine iliwaenelee na biashara ili
Mbeya irudi katika hali yake ya kilasiku