Picha ya pamoja na mgeni rasmi
|
|
IMEBAINIKA kuwa bado kuna ukatrili mkubwa wa kijinsia katika
familia za jamii ya kitanzania ambao unafanyika kimya kimya ambao huytokea
ndani ya nyumba kati ya mume na mke.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandolo
wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa waandishi wa habari kuriporti matukio ya
ukatili wa kijinsia ya siku nne kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Nyanda za
juu kusini yaliyo tolewa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania Tamwa.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya familia za kitanzania kuna
ukatili mbali mbali wa kijinsia ambao umekuwa ukitokea kimya kimya.
Aliutaja ukatili huio kuwa ni ukatili wa Kingono, ubakaji, kipigo
na ulazimishwaji wa mapezi kati ya wanandoa ambao umekuwa ukifanyika kisirisiri
katika familia.
Kandolo alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kufanya
utafiti wa ukatili wa aina hiyo na kuulipoti kisha kuielinisha jamii juu ya
ukatili wa aina hiyo ambao umekuwa ukinyanyasa mtu mmoja mmoja katika familia.
Alisema kuwa ukatili huo pia umekuwa ukitokana na mila na
destuli zilizopo katika jamii nyingi za kitanzania na waathilika wakuwa wakiwa
ni watoto.
Aliongeza kuwa katika utafiti uliofanywa na watu mbalimbali
kuhusiana na ukatili wa kijinsia unaofanywa katika ngazi ya familia umebaini
kuwa asilimia kubwa umekuwa katika mkoa wa Dodoma asilimia 71 huku mkoa wenye
ukatili kwa asilimia ndogo ni mkoa wa Tanga asilimia 16.
Kufuatia uwingi wa asilimia kubwa ya ukatili huo Serikali
imetengeneza mongozo wa kisera na
mwongozo wa kutoa huduma kwa waathilika wa ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya
watoto.
Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni
mhariri mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu alisema kuwa waandishi kama wataelimisha
jamii juu ya ukatili huo wananchi watajinasua katika ukatili huo.
Alisema kuwa kuwapo kwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia
kunaikwamisha nchi kusonga mbele kimaendeleo kwa ni wanaotendewa ukatili ni
wanawake kwa asilimia kubwa na wao ndio chachu ya maendeleo kwa taifa lolote
duniani.
Kwayu alisema kuwa katika taifa ambalo hakuna ukatili wa
kijinsia taifa hilo limesonga sana katika maendeleo yake.