JESHI LA POLISI LATOA TAMKO MCHEZO WA YANGA NA MBEYA CITY,


      • NI KUHUSIANA NA KILE KILICHO TOKEA UWANJANI 
        • GARI ZILIPIHWA MAWE
          • MASHINDANO YANAWEZA KUHAMISHWA MBEYA





WAKAZI wa jiji la Mbeya wanaweza kufukuza mashindano ya mpira wamiguu ligi kuu Tanzania kamawataendelea na tabia kwa Yanga siku ya mchezo wake na timu ya Mbeya City  mwishoni mwa wiki.

Hayo yamebainishwa na kamanda wa Pilisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman katika tangazo lake kwa umma alilitoa kwa vyombo vya habari.

Alisema kuwa mashindano hayo yanaweza kuota mbawa kama wakazi wa mbeya wataendelea na utovu wa nizamu kutoka na kile walichokifanya siku hiyo ya mechi katka uwanja wa Sokoine ambapo ulichezwa mchezo huo.

Athumani alisema kuwa watu wanao sadikika kuwa ni mashabiki wa timu ya Mbeya City walilipiga mawe gali la viongozi wea Yanga na kuvunja kioo cha gali hiyo cha nyuma.

Alisema gali hiyo ilikuwa imeegeshwa nje ya uwanja na mbali ya gali hilo la viongozi pia gari ya wachezaji pia ilipigwa mawe na mashabiki hao ambao walivunja kioo cha upande wa dereva.

Alisema kuwa kama hali itaendelea hivyo mashindano yataweza kuhamishwa mkoani  hapa na kuchezewa katika viwanja vingine nje ya Mbeya na kuwakosesha burudani wamenzi wa michezo.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani hapa halikulidhishwa na kuwapo kwa kwa vitendo hivyo kwani ni uvunjishu wa amani.

Alitoa wito kwa wakazi na mashabiki wa mpira wa miguu kuwa walizi wao wenyewe na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili kurahisisha kupatikana kwa wahalifu wa aina hiyo.