BODI YA MAJI KAZI KWENU


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Abas Kandoro  ameiagiza bodi mpya ya mamlaka ya maji safi na na usafi wa mazingira  iliyoteuliwa na waziri wa maji Jumanne Magembe, kuhakikisha wanaendeleza mazuri yaliyofanyawa na bodi iliyopita huku akitoa angalizo kwa bodi hiyo kuchapa kazi kwa vitendo badala ya kufanya kazi kwenye makararasi
Abas Kandoro,ametoa nasaha hizo pamoja na maagizo wakati akikabidhi mikoba yenye nyaraka za  miongozo ya kufanyia kazi  pindi  wanapotumikia bodi hiyo  kwa muda wa miaka mitatu  kuanzia julai 2013 hadi juni 2016.

Kwa upande wake mkurugenzi wa maji safi na majitaka mkoa wa Mbeya Mhadisi Simon Shauri amesema kuwa Pamoja na ongezeko la huduma ya maji  kwa wakazi wa Mbeya bado mamlaka ya maji safi na maji taka inakabiliwa na changamoto kubwa ya madeni sugu kutoka sekta za umma pamoja na tatizo la upotevu wa maji kutokana na sababu mbalimbali.

Mwenyekiti  mpya wa bodi hiyo  Jaji Atuganile Ngala akizungumza kwa niaba ya wajume wenzake wapya amesema kuwa wamezipokea nasaha hizo kwa moyo mkunjufu na kuahidi kushirikiana vema na bodi iliyopita pamoja na wananchi katika kutatua changamoto zilizobainishwa kuwa zinamalizika.
Habari na Furaha Eliabu Mbeya