WATANZANIA wa dini zote wametakiwa kuwa pamoja na kujadili
amani ya nchi yetu ambayo imeanza kuingia dosali kutokana na masuara ya udini.
Hayo yamebainishwa Juzi katika ibada ya Hija iliyofanyika
jijini Mbeya katika Kanisa la Familia ya Bikaila Maria wa Fatima, na Askofu wa
Kanisa katoriki Ask. Evaristo Chengla wakati wa ibada hiyo alisema kuwa
watanzania tokae pamoja na kujadili amani yetu.
Alisema kuwa wakatoliki wakae na wakristo wenzao ili
kuijadili amani inayo taka kuyeyuka na kukesha wakiomba amani ilejee kama
ilivyo kuwa katika miaka ya hapo nyuma.
Alisema amani hii inatoweka ni kutoka na kuzidi kuwapo kwa
maovu yanayo jitokeza katika mazingira yetu na kusengenya kumekuwa kwingi kwa
waumini wa makanisa yote wamekuwa wakiacha kusali na kujadili vitu vizivyo vya
msingi.
“Hamuwezi kupata amani pila ya kusamehe walio wakosea lazima
muwasamehe walio wakosea ndipo Mungu atawapatia neema ya amani, Amani ni Neema
tu kutoka kwa Mungu” alisema Ask. Chengula na kuongeza
“Amani tukiipoteza tutakuja kujuta tutaigumbuka hii tuliyo
nayo ni vema wakatoriki mkakaa pamoja na wakristo wengine na kujadiliana na
wenzetu juu ya amani tuliyo nayo ili tusije tukaipoteza”
Alisema mwaka huu kwa wakatoliki ni mwaka wa Imani waende wa
katende mema wakeshe wakiidumisha imani yao huku wakiiombea kwa pamoja amani ya
Nchi yetu na Upendo, Amani viwe pamija nao.
“Huu ni mwaka wa
Imani nendeni mkatende mema mkadumishe Upendo, Amani, Upananisho ikawe kaziyenu
popote muendapo hakika amani yetu iliyo ingia dosali itarejea” alisema ask. Chengula