KADI ZAGUSHIWA NA DOKTA AFIKISHWA MAHAKAMANI



WATU watatu wafanyakazi wa Hospitali ya binafsi ya Agha Khan ya Jijini Mbeya wamepandishwa Kizimbani, kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kugushi fomu za matibabu za Bima ya afya na kujipatia mali kinyume cha sheria.

Akisoma maelezo ya kesi mwendesha mashitaka wa Serikali, Achirosi Mlisa mbele ya Hakumu, Gilbert Ndeuruo wa Mahakama ya Hakimu mkazi ya Mbeya, aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Dk. Mashika Elineza (46), mhudumu wa Hospitali, Ally Hassan (40) wakiwa wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za makosa 264 na Nesi Advera Haule akiwa na anatuhumiwa kwa saba.

Alisema watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakiwa na tuhuma za gudushi fomu za matibabu za mfuko wa bima ya afya wa taifa (NHIF) ili wajipatie madawa bure katika maduka ya madawa.

Mlisa alisema kuwa watuhumiwa pia waligushi mihuri ya hospitali ya Rufaa na kudai malipo kwa NHIF wakidai wametoa huduma kwa mgonjwa mwanachama wa Bima.

Akisema maelezo ya mtuhumiwa wa kwanza Dkt. Elineza na wa pili Hassan alisema kuwa walifanya makosa hayo kwa nyakati tofauti katika kipindi Septemba na Novemba Mwaka jana wakiwa mkoani Mbeya.

Alidai kuwa watuhumiwa hao wawili waligushi fomu za NHIF kwa kudai kuwa walichukua dawa katika maduka mbalimbali ya mkoani Mbeya ikiwa ni katika maduka ya Babito, Mina, Bojan yote ya jijini mbeya na kudaidai Bima pesa za manunuzi ya dawa hizo.

Kutokana na udanganyifu huo wa kugushi na kusambaza nyaraka za matibabu zisizo harali ni kinyume cha kifungu cha kanuni ya adhabu cha 342 sura ya 16 kilicho fanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema watu kuwa watuhumiwa mbali ya kuchukua dawa kwanjia isiyo ya halali pia waligushi sahihi na muhuri wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoani  Mbeya na wakitumia madakrari wasio fahamika katika Hospitari hiyo.

Alidai kuwa walitumia majina hayo na kuwa wagonjwa ambao ni wateja wa NHIF walitibiwa katika hispitali hiyo ya Agha Khan kutoka Hospitali ya Rufaa na Kudai imesainiwa na madaktari hao ambao hawafahamiki katika hospitali ya Rufaa.

Watuhuniwa hao wanatuhumiwa kuchukuwa fedha za NHIF zaidi ya million 3.2 wakidai kuwa walichukua dawa katika maduka ya madawa na kuwatibu wagonjwa walio kuwa wakiandikiwa kutibiwa kutoka katika Hospitali ya Rufaa na kuja kutibiwa Hospitali ya Agha Khan ya jijini Mbeya.

Washitakiwa wote waponje kwa dhamana baada ya kukidhi vigezo vya kupata dhamana hiyo kutakiwa kurudi tena mahakamani hapo siku May 9 kwaajili ya kutajwa tena mbele ya Mahakama ya Makimu mkazi wa wilaya ya Mbeya hakimu Gilbert Ndeuruo.