MWAKA 1979 nikiwa ndani ya uwanja maarufu wa soka wa Dag
Hammaskjoeld katika jiji la Ndola nchini Zambia nilishuhudia (Taifa stars),
Timu ya taifa ya Tanzania ikilazimisha sare ya bao 1-1 kwa mwenyeji wake timu
ya Taifa ya Zambia (The KK-11).
Katika mchezo huo uliokuwa wa kufuzu kucheza fainali za
kombe la mataifa la nchi huru za Afrika na fainali zake kufanyika mwaka 1980
nchini Nigeria, huku Tanzania ikifuzu kwa mara ya kwanza, katika mchezo huo
ilisawazisha bao lililofungwa katika dakika ya 68 na Peter Tino bada ya wenyeji
kutanguliwa kupata bao dakika ya 29 lililofungwa na marehemu Alex Chola.
Nimelazimika kuanza na utangulizi huo kufuatia upotoshwaji
wa historia katika moja ya habari iliyoyotolewa katika gazeti maarufu la
michezo linalotoka mara mbili kwa wiki.
Baada ya kusoma habari iliyokuwa inaelezea inaelezea mchezo
huo mimi nikiwa kijana mbichi wa miaka 27 kwa wakati huo , nilishikwa na
mshangao kwamba Taifa Stars iliibuka kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Zambia
wakati habari hizo si za kweli .
Habari hizo zilizo kuwa na kichwa cha habari kilicho someka
kuwa ‘Peter Timo shujaa wa Taifa Stars aliye yumba kiuchumi-2 ’, ndiye aliye
kuwa muuaji wa Zambia baada ya kuifungia taifa Stars bao la pili na la ushindi.
Kutokana na ukweli kuwa historia ya mchezo huo imepotoshwa
bila kuathiri mukhutaza wa taifa stars kushiriki fainali za Nigeria, kwani kama
nilivyo eleza kwenye utangulizi wangu matokeo ya mchezo huo yalikuwa ni sare ya
kufungana bao 1-1.
Hivyo historia inabaki kuwa wazi tanzaia hajawahikuifunga
Zambia nyumbani kwake kwa muda wote na kwamba licha ya taifa stars kupata
matokeo ya sare iliweza kufuzu katik fainali hizo kwa faida za ushindi wa
mchezo wa awali wa nyumbani iliposhinda bao 1-0, lililo fungwa na Mchezaji
kiungo Adolph Rishad jijini Dar Es Salaam.
Kilichi nishangaza zaidi ni pale mchezaji mwenyewe Peter
Tino alipo koleza upotoshwaji huo kwa kusema kuwa aliifungia taifa stars bao la
pili kwa kichwa kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Hussein Ngulungu, baada ya
kuwazidi maarifa mabeki watatu wa Zambia na kuuweka mpira kimyani.
Mchezo huo uliochezwa Septemba 29, mwaka 1979 na kuhudhuriwa
pia na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zambia Kenneth David Kaunda daima utabakia
katika kumbukumbu za wazambia na wadau wengi wa mchezo huo, kutokana na
upinzani mkubwa uliokuwepo baina ya timu hizo mbili.
Uwanja huo uliopewa jina la katibu mkuu wa zamani wa umoja
wa mataifa kutoka nchini Sweden, Dag Hammarskjoeld ambao ulibomolewa na serikali mwaka 1990 kwa lengo
la kutaka kujenga uwanja mwingine, utabakia pia katika kumbukumbu ya wazambia
kutokana na timu yao ya taifa kutopoteza hata mechi moja kwa nchi za kiafrika
tokea nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa Muingereza Oktoba 24, 1964.
Kilichotokea siku huyo ni kwamba timu hizo zilitoka sare ya
bao 1-1 Zambia wakipata bao lao kutoka kwa Alex
Chola aliyepewa pasi na Godfrey Chitalu katika dakika ya 29 kipindi cha
kwanza, na Taifa Stars kusawazisha goli
hilo kupitia kwa Peter Tino katika dakika ya 68 kufuatia pasi murua ya Mohamed
Salim aliye ingia kuchukua nafasi ya Hussein Ngulungu.
Nilichogundua katika habari hiyo ni kwamba mwandishi
hakufanya utafiti wa kutosha baada ya kupewa taarifa za mchezo huo na mcheza sarakasi
aishie nchini Zambia Ramadhan Ngobariki,na ndio maana aliandia habari za
kupotosha kwani sidhani kama hata huyo aliye mpa hizo taarifa aliuona mchezo
huo.
Baadhi ya wachezaji kama Beki Leopard Mukebezi, marehemu
Juma Mukambi na Ezekiel Grayson (Jujuman), na Ahmed Amasha wanaotajwa
kuwa walicheza katika mchezo huo hawakuwemo katika timu iliyocheza mchezo huo.
Pia kwa upande wa Zambia waliwakosa wachezaji wao mahiri wa
enzi hizo kama Mlinda mlango Emmanuel Mwape, walinzi wa kutumainiwa Dick Chama,
Dickson Makwaza pamoja na washambuliaji hatari kama Obby Kapita, Brighton
Sinyangwe, Boniface Simutowe na Freddie Mwila ambao walikuwa wamestaafu soka.
Katika mechi hiyo taifa Stars iliwakilishwa na wachezaji:-
Juma Pondamali, Daudi Salum, Hassan Zitto/ Mohamed Kajole, Salim Amir, Leodgar
Tenga (Nahodha), Jella Mtagwa, Omary Hussein, Adolph Rishad, Peter Tino,
Hussein Ngulungu/ Mohamed Salim na Thuwen Ally.
Wachezaji wa akiba walikuwa makipa Omary Mahadhi na Idd Pazi
wakati wachezaji wengine walikuwa Leopard Mukebezi, Juma Mukambi na George Kulagwa.
Zambia iliwakilishwa na Vincent Chileshe, Benard Mutale,
Jack Simbule, John Yambayamba, Kampela Katumba , Moses Simwala, Pele Kaimana,
Jani Simulambo (Nahodha), Alex Chola, Godfrey Chitalu na Peter Kaumba.
Katika mchezo huo
Zambia walipiiga kona zipatazo 16 wakati taifa stars waliambulia kupata kona 3
tu.
Ujumbe ulioiwezesha taifa stars kufuzu kwa fainali hizo za
Lagos uliongozwa na waziri wa elimu na michezo wa wakati huo ambaye pia alikuwa
kiongozi wa msafara Chediel Yohana Mgonja, mwenyekiti wa FAT wa wakati huo Said
Hamad El-Maamry, Meneja wa Timu alikuwa Hadji Konde na waandishi wawili wa
habari Willy Chiwango (Daily news) na Salva Rweyemamu (Uhuru na mzarendo), na
mtangazaji wa Rtd Ahamed Jonga na fundi mitambo wake alikuwa Alfred Kunjumu
bila kumsahau balozi wa Tanzania nchini
Zambia kwa wakati huo.
Timu hiyo iliyo kuwa inafundishwa na kocha mkuu Slawomil
Voleck kotoka nchini Poland akisaidiwa na kosha mzawa aliyekuwa akiifundisha
majimaji ya Songea mkoani Ruvuma marehemu Raymond Gama, ilifikia katika hoteli
yenye nyota tano ya Savoi ambayo ipo katikati ya jiji la Ndola.
Mwandishi wa habari hizi anapatikana kwa simu Namba
0766-877649 au Barua pepe chandanews@gmail.com