SIKU chache baada ya kutokea kwa mlipuko wa Bom katika
kanisa katoriki la Arusha ulinzi umeanza kuimarishwa makanisani na kufanyiwa
upekuzi kwa watu wanaotiliwa shaka na waumini.
Hali hiyo imejitokeza
juzi katika ibada ya Hija iliyofanyika katika kanisa la Familia ya Bikira Maria
wa Fatima la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya Mzee Edward Mpeke Kutilia
mwandishi wa Tanzania Daima Jijini Hapa kuwa ni mtu mbaya kabla ya
kujitambulisha.
Mzee huyo akiwa na wenzake walianza kufuatilia nyendo za
mwandishi huyo baada ya kumtilia shaka na kutoa taarifa kwa kamati ya ulinzi
iliyokuwa ikisimamia ulinzi kanisani na kuanza umfuatilia mwandishi huyo.
Kutoka na ulinzi wa jeshi la Polisi kuimarisha uliznia wao
katisani hapo ambao walikuwa wametanda kila kona ya kanisa hilo huku misa iliyo
kuwa ikieneshwa na Askofu Evaristo Chengula ikiendelea walinzi hao walitoa
taarifa kwa Polisi.
Kwa ufuatiliaji wa kina Polisi waliona sio vema kumkurupusha
mtu huyo wanaye mhisi kuwa si mtu salama walitumia Askali kanzu ambaye
alimfuata Mwandishi huyo na kufanya mahojiano naye na kujitambulisha kuwa yeye
ni mwandishi wa habari na kuonyesha kitambulisho.
Askali huyo aliwatoa hofu walinzi wa kanisa hilo na kuaeleza
kuwa ni mwandishi wa habari ambaye yopo kazini lisha ya naye kusali katika
kanisa hilo la katolika katika Usharika Mwingine wa Sae Jijini Hapo.
Mwandishi huyo alisema kuwa aliwaona wazee hao wakumfuatilia
na kumpiga picha kitu ambacho yeye aliingiwa na wasiwasi na kumuuliza mzee huyo
kilicho endelea na kukosa jibu ndio akamuona askali kanzu akimhoji na kudai
kitambulisho kitu dipo alipo kuja kupata kilicho kuwa kikiendelea.
Kwa upande wa mzee huyo aliye onyesha ujasili wa kutoa
taarifa za mtu anaye mtilia shaka alisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo
kwaajili ya usalama wao wenyewe kitu ambacho kinapashwa kuwa chukuliwa mapema
kabla ya hatari.
Mzee Mpeke aliongeza kuwa maranyingi hatari inaweza kuzuiwa
ka kuchukuliwa hatua za awali kama hizo kwa mtuyeyote unaye mtilia shaka na
kutoa taarifa mapema.
Alitoa kwa waumini wa dini zote marazote wanapo muona mtu
wanae mtilia shaka iwe Msikitini, Kanisani ama mahara popote penye mkusanyiko
kutoa taarifa mapema ili kuweka mazingira salama.
Ibada hiyo ilianza kwa maadamano ambayo yaliongozwa na jeshi la polisi jijini Mbeya kutoka katika
kanisa kuu la Mkoani Mbeya hadi katika kanisa hilo la Familia ya Bikila Maria wa Fatima la
Mwajelwa jijini hapa.