Ligi
Kuu ya Vodacom inaendelea LEO (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili
zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya.
Yanga
itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa
Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu
Shooting.
Ligi
hiyo itaendelea kesho (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya
wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
WASHELISHELI KUICHEZESHA AZAM CAF
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Shelisheli
kuchezesha mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati
ya Azam na AS FAR ya Morocco itakayofanyika Aprili 20 mwaka huu Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
hao ni Emile Fred atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Steve Maire na
Jean Ernesta. Mwamuzi wa mezani (fourth official) atakuwa Jean Claude
Labrossa. Kamishna wa mechi hiyo ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda.
Wakati
huo huo, CAF imemteua Mtanzania Alfred Lwiza kuwa Kamishna wa mechi ya
kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Liga Muculmana
ya Msumbiji na Wydad Casablanca ya Morocco.