Lwiza |
MWANARIADHA wa zamani wa timu ya riadha ya taifa katika mbio
fupi na za kati (Short and Middle distance) Lwiza John, amesema kuwa anataka
kurudisha heshima ya mkoa wa Mbeya katika medali ya mchezo wa Riadha kwa kuibua vipaji vipya.
Akizungumza na Elimtaa hivi karibuni katika ofisi za
chama cha riadha zilizopo katika kumkumbukumbu ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, alisema kuwa
ameamua kufanya hivyo kwa sababu wachezaji wenye vipaji na uwezo wa kufanya
vizuri katika katika mmchezo huo.
Lwiza alisema kuwa kutokana na ujuzi na uzoefu alionao ameamua kuwasaidia vijana
hao chipukizia ili waweze kuutangaza Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla, kama
ilivyo tokea wakati wa kipindi chao kama wanariadha.
Lwiza ambaye ni mwalimu wa riadha wa mkoa wa Mbeya alisema kuwa
inasikitisha kuona mchezo huo unasusua katika Mkoa wa wakati siku za nyuma
ulitamba kwa kutoa wachezaji wengi wa riadha walio wakilisha kitaifa na
kimataifa na kuweka rekodi za taifa ambazo nyingine hazija vunjwa hadi leo
umepotea kabisa katika ramani ya mchezo huo.
Hata hivyo aliwataja wanariadha waliotamba katika mchezo huo
kuwanzia mkoa hadi taifa kuwa ni Genia Mboma, Nzaeli Kyomo, Mwinga Mwanjala,
Zaina Mwashambwa na John Wakachu Kadudu (Marathon).
Wengine ni Marehemu Erasto Zambi na Mariam Sadick, Ndege Makingi
(Kurusha Mkuki), Mwaijumba Kaparata, Mwakatwila, Seth Mwambapa, Mwakasata na
Lwiza John mwenyewe.
Bingwa huyo wa zamani wa mbio za mita 200, 400 na 800 hapa
nchini aliongeza kwa kusema kuwa ili kupata mafanikio katika kuufufua mchezo huu,
serikali pamoja na wabunge wake, viongozi na wadau wa mchezo huo lazima
tushirikiane kwa pamoja katika kuibua vipaji hivi pamoja na kuviendeleza.
Amependekeza kutumike mtindo wa zamani wa kuanzia michezo
katika shule za msingi, sekondari hadi vyuo kwa kuanzia ngazi za Vijiji, Kata, Tarafa,
Wilaya hadi Mkoa, ili kuweza kuwa na timu madhubuti iliyo bora na imara.
Pia amewataka wazazi wasaidie kuwaruhusu watoto wao ili
waweze kushiriki kimamilifu katika michezo ambayo baadaye inaweza kuja kuwapatia ajira.
Kwa mara ya mwisho mkoa wa Mbeya kufanya vizuri katika
riadha ilikuwa mwaka 2010 mpaka 2011 ulipojikusanyia medali mbili za dhahabu (Gold)
na moja ya shaba (Bronze), na kushika
nafasi ya tano kitaifa kati ya mikoa 25 ya wakati huo.
Mashujaa walio uletea medali mkoa wa Mbeya walikuwa ni Lwiza
John aliyeshinda medali mbili za dhahabu na mwenzake aliyemtaja kwa jina moja
la John, ambaye alitwaa medali moja ya Shaba katika kuruka vihunzi (huddles).
Na George Chanda, Picha na Mtandao