Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Baltazar Panklas Swai (49) mkazi wa Kitasha
Mengeni wilyani Rombo mkoani Kilimanajro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani
hapa kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tano mwenye matatizo ya
akili.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi
la Polisi iliyotolewa kwa waandishi habari inasema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Aprili
25 katika kijiji cha Aleni Chini.
Jeshi la Polisi mkoani
Kilimanjaro limesema kitendo hico kimemsababishia maumivi makali katika sehemu
zake siri.
Mwanafunzi aliyefanyiwa kitendo
hicho cha kinyama (14) ni wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mengeni
wilayani humo.
Imebainikia kwamba mwanafunzi
huyo ni mgonjwa akili na mbinu iliyotumika kumkamata mzee huyo ni ushirikiano
wa wananchi wa kijiji hicho kwa usimamizi wa Mwenyekiti Correntini Masawe.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema
mtuhumiwa pia ni mhalifu sugu kwani alishawahi kufungwa gerezani miaka ya nyuma
kutokana na matukio ya kihalifu huku
wakilaani kitendo alichokifanya mtuhumiwa na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua
mkondo wake.
Mwandishi:
YOHANA GERVAS
Mhariri: JOHNSON JABIR