WAZEE KUTIBIWA BURE MBEYA
SERIKALI imeanza kutimiza ahadi zake za kutoa huduma ya afya bure kwa wazee ambapo zaidi ya 190 zimetolewa kwaajili ya kupata huduma hiyo bure.
Afisa mtendaji wa kata ya Mabatini jijini Mbeya, Diaz Mzee Jana alisema kuwa wazee 197 wamepatiwa kadi za kwaajili ya kupatiwa huduma ya afya bure katika vituo vya afya.
Wazee hao watapata huduma hiyo bure katika vituo vya afya vilivyo jiunga na huduza za mfuko wa hifadhi ya jamii NHF mkoani Mbeya.
“Wazee 197 wamepatiwa kadi ambazo sasa waweza kutapata huduma ya wakati wowote watakapo ugua na zoezi hili ni endelevu na wazee wengine wanaendelea na usajili na watapatiwa kadi hizo.
Alisema wazee wanaendelea kujisajili katika mpango huo wa ambapo serikali inasaidia kutoa kadi hizo ambapo itasaidia kuondoa adha ya kupata huduma ya afya.
Alisema wazee walio pata kadihizo ni wa kutoka katika mitaa ya kata hiyo ya madatini ambayo ni mitaa ya Mianzini, Mabatini, Senjele, Simike, Kajigili ambao hutolewa kwa awamu.
Mzee alisema kuwa wazee wanaendelea kupatiwa kadi hizo huku wazee wengine wanaendelewa kujisajili na huduma hiyo na watapatiwa zikikamilika.
Alisema kuwa serikali inafanya utaratibu wa kuwaandikisha wazee wote na utaratibu huo unaendelea ambapo kila mzee atapatiwa huduma hiyo ya bure katika vituo vya afya.