KUFUATIA kuwapo kwa matatizo ya kiingeleza kwa wanafunzi wanapo ingia kidato cha kwanza shule zote mkoani Mbeya wanafundishwa lugha hiyo kwa muda wa miezi miwili ya awali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapa afisa elimu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda, alisema kuwa waafunzi wote wa kidato cha kwanza kwa mwaka huu watafundiswa kiingeleza kwa mda wa miezi miwili.
Alisema kuwa wanafunzi wanao anza kidato cha kwanza kwa mwaka huu wajifunza lugha ya kiingeleza kwa muda wa miezi miwili ili kuwawekea uwezo wa kuitambua lugha hiyo ambayo inatumika katika masomo katika shule za sekondari.
“Wanafunzi wote wa kidato cha kwanza mwaka huu wanapatiwa kozi ya kiingeleza kwa muda wa miezi miwili ambapo itawajenhea uwezo kwenye masomo yao ambayo yanafundishwa kwa lugha ya kiingeleza ambayo hutumika,” alisema Kaponda.
Alisema kwa kufanya hivyo wanafunzi watapata mwanga wa kwa kuijua vizuri lugha kwani wamekuwa wakitoka Darasa la Sabba ambako walikuwa wakifundishwa kwa lugha ya kishwahili na kuingia sekondari kwenye lugha ya kiingeleza kwa masomo yote.
Alisema mbali na kuwapatia wanafunzi hao elimu hiyo pia wamejipanga kukabiliana na changamoto ya kufeli kwa wanafunzi alisema kuwa mkoa umejipanga kufuatilia waalimu kwa ukaribu ufundishaji wao.
“Mkoa umemetoa agizo kwa waalimu kufuatilia kwa ukaribu wanafunzi wao na kufundisha kwa umakini na kuwasimamia wanafunzi kusoma kwani wasiposimamiwa wengi wao wanashinda kuchezea simu na kusahau kujisomea,” aliongeza Kaponda.
Alisema wanafuzi wa sasa wameasilika na teknilojia mara nyingi wamekuwa wakichati katika simu zao na wengine wakiwa katika kompyuta na kuchezea Intaneti.
Aidha Kaponda amewataka wanafunzi kujitahiti
na kujituma katika kujisomea na kuachana na mambo ambayo wanaona hayana manufaa
kwa masomo yao ili kupunguza asilimia za kufeli.