VIJANA mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza kwawingi
katika kushiriki michezo na mashindano mbalimbali yanayo anzishwa na wadau wa
michezo.
Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo wa halmashauri ya Jiji
la Mbeya, Vicent Msola wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashidano ya
baiskeli yaliyo endeshwa jijini Mbeya juzi.
Alisema kuwa vijana wakijitokeza katika michezo watapata
urahisi wa kupata ajira kwani michezo ni ajira na biashara pia ambaya inalipa.
Katika mashindao hayo ya kilomita 140 ambayo yalianza Mafiati
katikati ya jiji la mbeya na kuelekea Inyala kwenda na kurudi kwa baiskeli.
Mshindi katika mashindano hayo alikuwa ni Mashaka Jonas
ambaye alitumia masaa 3:47 kwa umali wa kilometa 140 na kujinyakulia kitita cha
shilingi laki 1.5.
Ambapo mshindi wa pili, Kiang Samson alitumia masaa 3:59
na kujinyakulia kitita cha shilingi laki 1 na mshindi wa pili alikuwa, Jonas
John ambaye alitumia masaa 4:11 kwa umbali ule ule alijishindia kiasi cha
shilindi 50,000.
Katika mashindano hayo zawadi zilitolewa kwa washindi watatu
wa awali, mratibu wa mashindano hayo Patrick Kahise alisema kuwa kumekuwa na
changamoto mbalimbali katika maandalizi ya mashindano hayo.
Alisema kumekuwa na ugumu wa uendeshaji wa mashindano
hayo kutoka na wadau kuto jitokeza katika kuchangia uendeshaji wa mashindano.
Mashindano hayo hayajaendesha mkoani Mbeya kwa mda mrefu
zaidi ya miaka minne na kuonekana kuwa na muitikio mdogo kwa wadau wa wachezaji
wenyewe.
Waendesha baiskeli 16
walishioliki mbio hizo za kilomita 140 na kupatikana washindi watatu ambao
walipatiwa zawadi na wengine kupatiwa vifuta jasho.