WARATIBU WATAKIWA KUSIMAMIA WAALIMU



WARATIBU elimu kata wametakiwa kuwasimamia waalimu waendapo kufundisha na kuwa navitendea kazi ambavyo anapashwa kuingia navyo darasani.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandolo aliyasema hayo juzi katika kikao cha Afisa elimu wa Mkoa wa Mbeya na maafisa elimu wa wilaya na kata kilichokuwa kukilenga uboreshaji wa kazi.

Alisema kuwa kamwe wasimruhushu mwalimu kuingia darasani bila ya kuandaa kumbukumbu za vitu atakavyo vifundisha darasani za kujifunzia.

Alivitaja baadhi ya vitu ambavyo waajimu wanavyo takiwa kuwa navyo ni pamoja na Maadhimio ya Kazi, maadalio ya somo nukuu za somo utoaji wa mazoezi kwa wanafunzi na kazi za nyumbani.

Walatibu elimu wa kata wanatakiwa kuhakikisha wanafuatilia waalimu kuwa na vitu hivyo nah ii isasaidia kuwa na ufundishaji ulio bora na kusaidia wanafunzi kuelewa kwani watafundishwa kwa mfumo mzuri.

“Jambo la kusikitisha ni uzoefu unaonyesha kuwa waratibu elimu wa kata hamuwajibiki kikamilifu wengi hamtembelei shule lisha ya idadi ndogo ya mlizo nazo,” alisema Kandolo.

Alisema inasikitisha kuwa kumekuwapo kwa shule chache ambazo waratibu elimu wanasimamia lakini huwa hawafiki kuzitembelea shule hizo mara kwa mara.

Aidha aliongeza kuwa ni vema mratibu wa elimu afuatilie uwapo wa ratiba ya masomo, na kazi za nje pamoja na mgawanyo wa majukumu na idara za masomo na bodi ya shule katika jengo la utawala.

Endapo yote haya yatafuatiliwa elimu itapanda juu na kuepukana na aibu ya kufeli iliyo ilikumba taifa kwa matokeo ya wanafunzi waliofanya mtihani mwaka jana.