UDINI NI SUMU



UDINI ni sumu mbaya kwa taifa zaidi ya ile ya umaskini kwani na inaweza kusababisha taifa kuingia katika vita na kukimbiza wafadhili
na wawekezaji hapa nchini.

Mbali na kuvuruga nchi pia unaweza kuharibu maendeleo ikiwemo na
ushirikiano kwa wanafuni katika kujisomea na wanafunzi kujigawa
shuleni.

Akizungumza katika wakati wa ufunguzi wa hosteli ya wasichana  katika chuo cha ufundi Moroviani Mbeya, makamu mwenyekiti wa kanisa Moroviani
Duniani, Mchungaji Nosigwe Buya, alisema kuwa kukiwepo na vurugu hapa nchini tunaweza kupoteza wawekezaji kutoka nchi za nje.

Alisema kuwa udini ni sumu mbaya ambayo inaweza kuligawa taifa na kusavita mbayo ni mbaya kuliko vita nyingine yeyote.

Alisema wazazi waache kuwapotosha watoto wao kuhusiana na mambo ya kidini kwani wanapandikiza roho mbaya ambayo baadae itakuwa na madhara makubwa kwa taifa letu.

“Zamani watanzania tulikuwa tunajua huyu ni Dini fulani wakati anaenda kusali siku ya ibada lakini tulikuwa tukishiriki mambo mengi pamoja
bila ya kuuliza dini” alisema Mchungaji Buya.

Aliongeza “Sumu ya udini ni mbaya kuliko ya umaskini kwa ni ya umaskini munaweza mkakaa pamoja na kujadili jinsigani ya kukabiliana
nayo hii sumu hamuwezi mkakaa pamoja na kujadili kinacho wasibu pia nawashukuru walio enda kuomba ili kupambana na masuala haya ya udini hapa nchini,”

Walio kaa na kuombeya suala huli la udini wamechukua uamuzi wa busala na nivizuri kwani hawakuchukua uamuzi wa kulipiza kisasi na kisasi
chamungu hakipo kumuadhibu adui yako kipo kukulinda wewe na adui yako.

Alisema watanzania wafuate Mungu anasema nini sema nini na tutakuwa na amani yetu ile ya awali irudi na tuishi kama zamani kwani sisi ni
ndugu na tunajenda taifa moja.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dakt. Norman Sigalla alisema kuwa serikali ya mkoa imekaa na pande zote mbili na kuzungumzia suala hilo linalo taka kuivuruga amani nchi yetu.

Alisema kuwa ukusema dini furani ni mbaya si waanini wote wa dini ile ni wa baya, hivyo serikali imepiga marufuku usabazaji wa kanda za
zinazo sema ubaya wa dini na kwa bahati mbaya kanda hizo hazitengenezwi Mbeya na zinadaiwa kutengenezwa Jijini Mwanza.

“Serikali ya mkoa wa Mbeya imepiga marufuku usambazaji wa kanda zinazo onyesha didi moja mbaya na kwabahati mbaya kanda hizo hazitengenezwi hapa Mbeya na zinatengenezwa Jijini Mwanza, na kwa mtu yeyote atakayekamatwa atakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria iwe anasikiliza nyumbani ama popote pale atakamatwa,” alisema Dakt.
Sigalla

Jengo hilo la Hosteli ya wasichana imejengwa kuwa ufadhili wa familia ya Dr. Worwag ambayo inaishi nchini Ujerumani na limejengwa Robo ya
jingo zima na imegharimu zaidi ya Shilingi 309.7 na linaendelea kujengwa.

Nae Dr. Worwag alisema uzinduzi wa jingo hilo unatia faraja na kutapatikana idadi ya wasichana wengi wanao soma na aliwatakiwa mafanikio katika masomo yao na katika maisha.