WAALIMU WAFIKISHWA MAHAKAMANI NI KWA TUHUMA ZA RUSHWA








WAALIMU wawili wa shule ya sekondari ya Forest ya Jijini Mbeya waliokamatwa na taasisi ya kubambana na Rushwa (Takukuru) jana wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma 16 za kushawishi wanafunzi kutoa rushwa.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu mfawizi wa bahakama ya mkoa wa Mbeya Michael Mteite, mwendesha mashitaka wa Takukuru, Nimrod Mafwele, alisema kuwa waalimu hao wawili walitema makosa hayo Machi 4  mwaka huu wakiwa katika shule ya sekondari Forest jijini Mbeya.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mwalimu, Faustini Robert na Solomon Joseph ambao walifanya ushwawishi kwa wanafunzi 16 watoe hongo ili wasamehewe makosa mbalimbali yakiwemo ya uchelewaji shuleni.

Watuhuniwa hao wali kuwa wakipokea hongo kutoka kwa wanafunzi ambapo ni kinyume cha kifuingu namba 15 na kifungu kidogo cha 1 (a) cha mwaka 2007, sheria namba 11 

Alisema waalimu hao walikutwa na makosa 16 ya kuwashawashi wanafunzi 16 wakiwa na makosa tofati wa shule hiyo ya ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa wakichelewa kwenda shuleni.

Akisoma kosa la kwanza kwa watuhumiwa hao alisema watuhuniwa walishawishi hongo ya shilingi 500 kutoka kwa wanafunzi, Samweli Elias, kidato cha nne, Evalina James, kwa kosa la kuchelewa shuleni ili asichapwe viboko.

Mbali na kushwashishi pia walipokea hongo ya shilingi 300 kutoka kwa mwanafunzi Evalini kwa kosa la kuchelewa fika shule badala ya vioboko kwa mwanafunzi huyo.

Katika kosa namba 15 alisema kuwa waalimu hao kwa pamoja walipokewa hongo ya shilingi 1000 kutoka kwa Mika Kalua kwa kosa la kuvaa viatu ambavyo havitakiwi shuleni hapo.
 
Kulingana na makosa hayo watuhumiwa wanaweza kudhanimika kama watatimiza masharti ya dhamani ambapo hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Hakimu Mteite alitaja masharti mawili tofauti ya dhamana hiyo kuwa ni watu wawili mmoja akiwa na hati ya Nyumba na wapili akiwa na barua kutoka kwa mwajili.

Alisema sharti la pili ni kuweka pesa Benki zenye thamani ya shilingi milioni 2, watuhumiwa hao  walichagua sharti la kwanza na walirudishwa mahabusu mpaka watakapo kamilisha masharti hayo.
 
Mteite alisema kuwa kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Aprili 10 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza kesi hiyo.

*Samahani kwa picha mbaya picha: watuhumiwa ni Faustin Robert aliyevaa shati Nyekundu, na aliye vaa koti na shati ya kijani ni Solomon Joseph*