LICHA ya Serikali
kupunguza kiwango cha vocha za mbolea ya ruzuku kutoka 835,000 kwa mwaka wa
2011/12 hadi vocha 7,973 za pembejeo zilizofika Wilayani Kyela kwa mwaka huu
zimedoda baada ya wakulima kushindwa kuzichangamkia ili waweze kuzitumia katika
kilimo cha mwaka 2013 ukilinganisha na mwaka jana.
Akizungumza
na mtendaji wa halmasharuri ya wilaya ya Kyela, Abdarah Mfaume alisema
kuwa sababu inayosababisha wakulima kutojitokeza kwa wakati katika
kujiunga na mpango wa mbolea za ruzuku ni kutokana na uwezo mdogo wa kuchangia
bei za pembejeo.
Alisema kuwa
pamoja na serikali kumchangia mkulima sh,50,000,na mkulima mwenyewe kutoa sh, 26,000,
lakini bado muitikio wa wakulima hao kuzichangamkia mbolea hizo ni mdogo na
kuwa hadi sasa vocha bado zipo kwa baadhi ya maeneo,
“Ni kweli mwaka
huu vocha zilifika chache ukilinganisha na mwaka jana lakini bado utokaji wa
vocha hizo ni wakusuasua hii inatokana na wakulima kutojipanga vizuri kwa ajili
ya kilimo na ndiyo maana baadhi yao
wameshindwa kuchangia gharama hizo” alisema Mfaume.
Alisema kuwa licha
ya vocha hizo na mbegu kuwahi kuwafikia na Serikali kupunguza bei yake ya
kununulia lakini mwamko wa kwa wakulima kuzinunua vocha hizo umekuwa ni mdogo sana kwa kuwa ziifika
chache na bado zimebaki nyingi.
Aidha Mkurugenzi
huyo alizitaja changamoto zilizo changia mkulima kutozichangamkia vocha hizo ni
pamoja na ushirikiano mdogo kati ya kamati ya vocha ya kijiji na ya kata jambo
lililopelekea baadhi ya wakulika kuacha kuchukua vocha kutokana na
ucheleweshaji wa kamati hizo.
Aliongeza kuwa
ugeni wa zoezi la kutumia makampuni badala ya mawakala kama
ilivyo zoeleka ni moja ya sababu iliyopelekea wakulima kutojitokeza kuchukuwa
vocha hizo.
Baadhi ya wakulima
waliozungumza na Gazeti hili kwa kutotaja majina yao walisema kuwa tatizo lililopo ni kwamba
serikai licha ya kupunguza hata hivyo bado haiendani na hali haisi ya
watanzania kwa sasa.
Walisema kuwa
maisha yamekuwa magumu bei ya vyakua vimepanda kwa kasi kubwa hivyo wakulima
wamekuwa wakipata changamoto kubwa pindi zinapofika vocha hizo kutokana na
kukabiliana na mambo mengi ya shule na mambo mengine.
Aidha waliongeza
kuwa ni vyema serikali ikaanzisha utaratibu wa ugawaji mbolea kipindi cha mwezi
Juni au Julay kwa kuwa kipindi hicho ndicho wakulima wanakuwa na chakula kingi
na pesa zinapatikana kuliko kipindi ambacho wengi wanakuwa wamezitumia katika
mambo yao mbali
mbali.