FUATENI WAHUSIKA



WAWEKEZAJI na taasisi zinazo jihuisisha na huduma kwa jamii zinapo kwa ma katika mambo yanayo ihusu serikali waende kwa serikali wilaya au ya mkoa ili kuepuka mrorongo mrefu.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dakt. Norman Sigalla aliyasema hayo juzi wakati akizindua bweni la wasichana wa chuo cha Moraviani Mbeya, alisema kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikikwama kukamilisha usajili kutokana na kutoenda kwa wahusika wa suala wanalolihitaji.

Aliyasema hayo baada ya makamu mwenyekiti wa kanisa Moraviani Duniani Mch. Nosigwe Buya kutoa malalamiko ya kusumbuliwa wakati wakifuatilia kibali cha uanzishwaji wa chuo wakati akitoa hutoba yake.

Dakt. Sigalla alisema kuwa kwa masuala ya ufunguzi wa taasisi mbalimbali inapaswa kuuona uongozi wa juu ili kuepukana na mizunguko mingi ya kupata hati za kufungua taasisi zao.

Awali Mch. Buya alisema kuwa wamekuwa wakipata shida katika ufunguzi wa taasisi za kijamii hasa katika usajili na kupata vibali vya ufunguzi wa wake.

“Tumekuwa tukisumbuliwa na wakaguzi ambao wanakaguwa majengo kabla ya kufungua taasisi ambapo wamekuwa wakihitaji vitu vingi na vingine visivyo na msingi wowote na maranyingine wamekuwa wakigongana kutoa masharti ya ufunguzi na uanzishaji wa taasisi,” alisema Mch. Buya.

Alisema wakati wakitaka kufungua taasisi ya ualimu walipatashida na kudaiwa vitu vingi bado hawaja kamilisha  na kutakiwa wavikamilishe vitu ambavyo havikuwa na sababu ya kuzuiwa kupewa usajili na uanzishwaji wa chuo.

“Vivyo hivyo wakati wa ufunguzi wa chuo cha uuguzi tuliambiwa tuwachukue wanafunzi wenye alama ‘D’ moja au mbili achukuliwe lakini baada ya kuwachukuwa na wakiwa wamesoma zaidi ya miezi sita tukaambiwa wanao takiwa ni waliopata alama ‘D’ tatu ndio wanahitajika kusoma,” aliongeza Buya.

Alisema kuwa serikali nivema ikawa wazi kwa taasisi zinazo saidia jamii kwa kuzipunguzia masharti na kwani watoto wengine wasinge pata nafasi ya kusoma katika vyuo vya serikali na taasisi hizo zinawapatia elimu.